Rais Samia atoa maagizo kwa uongozi wa ALAT

Na Doreen Aloyce, Diramakini blog

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suuhu Hassan ameutaka uongozi mpya wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) kuanza kutumia mfumo wa TEHAMA, katika kutekeleza majukumu yake hususani kwenye ukusanyaji wa mapato ya Serikali ili kuhakikisha wanadhibiti upotevu wa fedha ambazo zimekuwa zikipotea kila siku.
Rais Samia amesema hayo leo Septemba 27,2021 wakati akifungua mkutano mkuu maalum wa uchaguzi wa viongozi wa jumuiya hiyo uliofanyika jijini Dodoma.

“Twendeni tukasimamie vizuri mapato yetu ya ndani kwa kila halmashauri zetu ni ukweli usiopingika fedha tunazokusanya kwenye halmashauri ni kidogo.

"Nchi yetu imekuwa ikikumbwa na migogoro mingi ya ardhi na yote hayo ni kwa sababu hakuna kumbukumbu sahihi kwenye mamlaka zetu tunazofanyia kazi na hili liko wazi kumukumbu sahihi tutazipata tu pale tutakapoanza na kujikita na kutumia mifumo ya Tehama ,”amesema Rais Samia.

TOZO

Ameagiza fedha zote zilizokusanywa kwenye miamala ya simu kama tozo walizokuwa wakikatwa wananchi kwenda kujenga madarasa huku akisema naye ataongeza fedha ili yajengwe madarasa 15,000 ili kuwezesha wanafunzi watakaochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza kuanza wote kwa pamoja mara shule zitakapofunguliwa.

“Kumekuwa na uhaba mkubwa wa madarasa hivyo basi naelekeza fedha hizi ziende kujenga madarasa,na mimi kuna hela nimeipata pahala tutashirikiana ili kuwezesha ujenzi wa madarasa hayo,”amesema.

CORONA

Rais amewaagiza Mameya,Wenyeviti wa Halmashauri na Wakurugenzi wa majiji ,miji na halmashauri kushirikiana kwa kuwahamasisha wananchi kwenda kuchanja chanjo ya ugonjwa wa Covid-19 .

“Kumekuwa na migongano kati yenu kwani kunabaadhi wanataka wananchi wakachanje na wengine hawataki wananchi wakachanje sasa wote muwe kitu kimoja uhaamasishe wananchi wakapate chanjo ya Corona 19,”amesema Rais Samia.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Ofisi ya Tamisemi imekuwa ikitekeleza miradi mingi ya kimaendeleo na miradi hiyo imekuwa ikipitishwa na madiwani.

Naye Spika wa bunge la Tanzania, Job Ndugai amezitaka kila halmashauri kukusanya fedha za miradi za maendeleo kwa asilimia 40.

“Hatutaivumilia halmashauri yoyote itakayoleta makusanyo ya fedha za maendeleo chini ya asilimia iliyowekwa iwe asilimia 40 au asilimia 60 makusanyo hayo lazima yapatikane,”amesema Ndugai.

Naye Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Ummy Mwalimu ameishukuru serikali kwa kuendelea kutoa fedha za kutosha ili kukamilisha miradi ya kimaendeleo.

Pia amemshukuru Rais Samia kwa kuwapa thamani madiwani kulipwa posho kila mwenzi jambo alilisema itapunguza manun’guniko kwa madiwani hao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news