Taasisi ya Al - Wadoud yawapa faraja watoto yatima

Na Anneth Kagenda

JAMII imetakiwa kuhakikisha inawasaidia watoto yatima nchini hasa wale wanaolelewa katika vituo vya kulea watoto katika maeneo mbalimbali kwa madai kuwa kujitolea kuwasaidia watoto wadogo ni thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Hayo yamesemwa Dar es Salaam na Uongozi wa Taasisi ya Al - Wadoud yenye makazi yake nchini Omany kupitia kwa Mwenyekiti wake Sheikh Abdul Qader Al Jahdhamy, pamoja na Uongozi wa Tanzania Peace Foundation (TPF-TY), kupitia kwa Mwenyekiti wake Edward Mwenisongole wakati wakikabidhi msaada wa vyakula kwa Kituo cha kulelea watoto Yatima cha Maunga Orphanage Centre kilichopo Kinondoni Mkwajuni chenye watoto zaidi ya 48.

Mwenyekiti Sheikh Al Jahdhamy amesema kuwa, ni wakati mwafaka kwa jamii mzima kuhakikisha wanawasaidia watoto yatima na hasa wale walioko kwenye vituo vya kulelea yatima kwani kufanya hivyo ni kupata dhawabu kwa Mungu.
"Lakini pia ijulikane kwamba suala lingine ni kwamba watoto hawa ndio Taifa na viongozi wajao, hivyo kila mmoja kwa nafasi yake kwenye jamii hana budi kuona umuhimu wa kuwasaidia watoto hawa,"amesema Kiongozi huyo.

Naye Mwenyekiti Edward Mwenisongole amesema, taasisi hiyo ipo kwa ajili ya kuhubiri amani kwa Taifa la Tanzania na kuhakikisha wananchi wanaishi kwa kupendana.

"TY Mkoa tunalojukumu kubwa la kueneza upendo na amani kwenye nchi yetu na pia suala la kuwasaidia na kuwalea watoto yatima ni la kwetu, hivyo watoto hawa wakikosa amani ni moja ya sababu inayoweza kupelekea pia kuwepo kwa vurugu hivyo jamii tunatakiwa kushirikiana,"amesema Mwenyekiti Mwenisongole.

Mwanzilishi wa Kituo hicho Zainabu Maunga, alitoa shukrani zake za dhati kwa uongozi mzima wa TPF, TY ,TW na Uongozi wa Taasisi ya Al- Wadoud kwa msaada huo mkubwa kwa watoto wake ambao alisema kuwa kwa kiasi kikubwa utawasajdia watoto hao.

Amesema pamoja na mambo mengine kituo chake kimekuwa kikikabiliwa na changamoto mbalimbali kubwa ikiwa ni bili za umeme, maji uhaba wa vyakula na kwamba anatamani watoto hao wangejengewa kituo kikubwa cha kulelea watoto hao.

"Nashukuru sana kwa misaada hii kutoka kwenye taasisi zote lakini niiombe jamii iendelee kujitolea kuwasaidia watoto hawa kwani mnawaona walivyokuwa wadogo na wanatakiwa mahitaji mbalimbali,"amesema Bi Zainabu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news