BREAKING NEWS:Haji Manara aandaa jopo la Mawakili 10 kuuburuza uongozi wa Simba SC mahakamani

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amesema kuwa, ameandaa jopo la mawakili 10 ambao wamejiandaa kuifungulia kesi Klabu ya Simba ili aweze kulipwa madai yake.

Haji amesema kuwa, ndani ya utumishi wake katika klabu hiyo ya zamani akiwa Msemaji alitumikishwa bila mkataba na aliondoka kwa kutengezewa zengwe hivyo anakwenda mahakamani ili alipwe gharama zote.

"Ninaidai ile klabu fedha nyingi sana, hivyo jopo langu la mawakili lipo mbioni kwa ajili ya kufanya jambo ili tuweze kuchukua hatua,nina mambo mengi sana ambayo nilifanyiwa nikiwa ndani ya Simba SC, lakini mimi nina kifua ndiyo maana nimejaribu kuvumilia, lakini nimekuwa nikichokozwa,"amesema.

Manara ameyasema hayo leo Oktoba 13, 2021 wakati wa mahojiano maalum katika kipindi cha LaviDavi kinachorushwa na Wasafi Redio na Mtangazaji Diva the Boss lady.

Post a Comment

0 Comments