NECTA yafuta matokeo yote ya watahiniwa 393 Mtihani wa Darasa la Saba 2021

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), limefuta matokeo yote ya watahiniwa 393 waliobainika kufanya udanganyifu katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa mwaka 2021.Matokeo yote soma hapa>>>
Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dkt. Charles Msonde ameyabainisha hayo leo Oktoba 30,2021 wakati akitangaza matokeo.Wanafunzi 10 Bora soma hapa>>>

Amesema, baraza limezishauri mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua kwa mujibu wa kanuni za utumishi na sheria za nchi wale wote waliohusika ama kusababisha kutokea kwa udanganyifu huo.

Katika hatua nyingine, Msonde amesema pia baraza limezuia kutoa matokeo ya watahiniwa 128 ambao waliugua au kupata matatizo na kushindwa kufanya mtihani kwa masomo yote au baadhi ya masomo.

Amesema watahiniwa hao wamepewa fursa nyingine ya kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa mujibu wa kifungu 32(1) cha kanuni za mitihani.

Dkt. Msonde akizungumzia ufaulu amesema kwamba, idadi ya watahiniwa waliofaulu kwa mwaka 2021 imeongezeka kwa watahiniwa 74, 130 sawa na asilimia 8.89 ikilinganishwa na mwaka 2020, ambapo somo la Kiswahili limeongoza kwa wanafunzi kufaulu huku ufaulu katika somo la Kiingereza ukishuka na kuwa na asilimia 48.02.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news