Bosi wa TIC mguu kwa mguu hadi kwenye miradi ya uwekezaji

NA MWANDISHI MAALUM

MKURUGENZI Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt. Maduhu Kazi amefanya ziara katika Mradi wa Kuzalisha Vifaa vya Umeme (Electrical Products) wa Kampuni ya ELSEWEDY ELECTRIC EAST AFRICA LTD na kupokelewa na meneja wa mradi huo, Dkt. Ibrahimu Qamar maeneo ya Kigogo Kisarawe II Manispaa ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam.
Dkt.Maduhu ametembelea mradi huo Novemba 25,2021 ili kujionea hatua ya ujenzi ilivyofikia. 

"Nimekuja kuona mnaendeleaje na ujenzi na nimefurahi kuona hadi sasa mmefikia asilimia 93 kama Dkt. Ibrahimu alivyosema mjitahidi mmalizie haraka kazi iendelee hongereni sana,"amesema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Dkt. Maduhu Kazi, wa pili kulia, akipatiwa maelezo na Meneja mradi Dkt. Ibrahimu Qamar katika Mradi wa kuzalisha vifaa vya Umeme (Electrical Products) wa Kampuni ya ELSEWEDY ELECTRIC EAST AFRICA LTD uliopo Kigogo Kisarawe II Manispaa ya Kigamboni leo tarehe 25 Novemba, 2021.

Nae Dkt. Ibrahimu amesema kwa sasa kampuni ipo kwenye hatua za mwisho za ufungaji wa mashine 15 walizopokea na kukamilisha ujenzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Dkt. Maduhu Kazi, wa pili kutoka kushoto, akipatiwa maelezo na msimamizi wa mradi Bw. Mahmoud Abobakar, wa kwanza kushoto, kuhusu maendeleo ya mradi alipotembelea eneo la INDUSTRIAL PARK lililipo Kigogo Kisarawe II Manispaa ya Kigamboni, ambapo kampuni ya ELSEWEDY ELECTRIC EAST AFRICA LTD itatekeleza uwekezaji huo.

Wakati huohuo Dkt. Maduhu ametembelea eneo la mradi wa INDUSTRIAL PARK lililipo Kigogo Kisarawe II Manispaa ya Kigamboni ambapo kampuni ya ELSEWEDY ELECTRIC EAST AFRICA LTD itatekeleza uwekezaji huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Dkt. Maduhu Kazi na wafanyakazi wa mradi wa kuzalisha vifaa vya Umeme (Electrical Products) wa Kampuni ya ELSEWEDY ELECTRIC EAST AFRICA LTD uliopo Kigogo Kisarawe II Manispaa ya Kigamboni leo tarehe 25 Novemba, 2021.
Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Dkt. Maduhu Kazi, alipotembelea eneo la INDUSTRIAL PARK lililipo Kigogo Kisarawe II Manispaa ya Kigamboni, ambapo kampuni ya ELSEWEDY ELECTRIC EAST AFRICA LTD itatekeleza uwekezaji huo leo 25 Novemba, 2021.

Dkt. Maduhu amewapongeza kwa hatua nzuri waliyofikia na amewaeleza kuwa kama kutakuwa na changomoto zozote kwenye kutekeleza mradi wao wasisite kuziwasilisha TIC kwa ajili ya kuzitatua.

Post a Comment

0 Comments