Diamond Platnumz aonyesha kufuru ya fedha, anunua pete na bangili kwa Milioni 600/-

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

STAA wa Bongo Fleva na Mkurugenzi Mtendaji wa Wasafi Classic Baby (WCB), Nassib Abdul Juma (Diamond Platnumz) ameendelea kuonyesha jeuri ya fedha baada ya kuanika vito vipya vyenye thamani ya Shilingi Milioni 600 za Kitanzania.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Diamond Platnumz ameweka picha kadhaa zinazoonesha baadhi ya sehemu za mwili wake hasa mikono ikiwa imepambwa kwa vito hivyo vya thamani ambavyo ni pete zilizoenea kwenye vidole vyake vyote vya mkono zikiwa na maneno yenye kusomeka SIMBA.

SIMBA pia ni jina lake analoitwa kutokana na mambo makubwa anayoyafanya kupitia muziki huo.
Diamond Platnumz ameweka wazi kuwa, imemgharimu kiasi cha pesa kisiachopungua Dola za Kimarekani 100,000 ambazo ni sawa na Shilingi Milioni milioni 230 kununua pete alizovaa pekee.

Huku bangili zikiwa zimemgharimu Dola 117,000 sawa na Shilingi Milioni 407 za Kitanzania.
Hii si mara ya kwanza kwa msanii Diamond Platnumz kuonyesha bito vya thamani ambavyo amekuwa akinunua.

Diamond Platnumz, mara ya mwisho ni takribani mwezi mmoja uliopita alipoonyesha saa yake mpya aina ya Rolex yenye thamani ya dola za Kimarekani 30,000 ambazo ni sawa na Shilingi Milioni 69 za Kitanzania.

Post a Comment

0 Comments