KATIBU MKUU CHONGOLO AITAKA UVCCM KUACHA KUWA WAPAMBE BINAFSI WA VIONGOZI

NA MARY MARGWE

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Daniel Chongolo ameutaka Umoja wa Vijana (UVCCM ) kuacha tabia ya kuwa wapambe binafsi wa viongozi, na badala yake waelekeze nguvu kazi kujenga miundombinu ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
Katibu Mkuu huyo ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa ambavyo vinajengwa kwa nguvu ya umoja wa vijana wa CCM katika shule ya Bukama, kata ya Kagoma wilayani Muleba mkoani Kagera.

Chongolo alisema lengo ya kuanzisha umoja wa vijana haikuwa na maana ya kuwatumia vijana hao kwenye mambo ya kutafuta kura za wagombea na kuhangaika na masuala binafsi ya viongozi, bali ni kujenga nchi kwa kujitolea na baadae kupata fursa ya kwenda kulitumikia Taifa kwa faida yao na nchi.

Kufuatia hilo amewataka viongozi wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanatumia Umoja wa Vjana wa chama hicho kujenga miundombinu pamoja na miradi ya maendeleo wanayoanzisha kwenye maeneo yao, na sio kuwa wapambe binafsi wa viongozi, hivyo ni vema UVCCM wakalitambua hilo.

"Malengo ya kuanzisha Umoja wa Vvijana haikuwa na maana ya kuwatumia vijana hao kwenye mambo ya kutafuta kura za wagombea na kuhangaika na masuala binafsi ya viongozi, bali ni kwa ajili ya kujenga nchi yetu kwa kujitolea na baadae kupata fursa ya kwenda kulitumikia Taifa kwa faida yao na nchi yetu kiujumla,"alisema Katibu Mkuu huyo.

Aidha,alifafanua kuwa miaka ya nyuma kazi ya Umoja wa Vijana (UVCCM ) ilikuwa ni kujiitolea kujenga miundombinu na kufanya mambo mengine ya maendeleo na baadae kupata fursa ya kwenda jeshini kulitumikia Taifa kwa faida yao na nchi kwa ujumla.

“Miaka ya 2000 nyuma, asilimia 90 ya vijana ambao walikuwa wanachukuliwa kwenda jeshini walikuwa wanatokana na Umoja wa Vijana ni kwa sababu walikuwa wanajitolea kulitumika Taifa kwa kupitia Umoja huo,” amesema.

Aidha, aliongeza kwa sasa vijana wengi wa umoja wa vijana wamekuwa wapambe namba moja wa wagombea na waangaikaji wa mambo binafsi ya viongozi huku wakiacha majukumu yao halisi.

Katika hatua nyingine Chongolo amewapongeza umoja wa vijana Wilaya ya Muleba kwa kujitolea kujenga vyumba vya madarasa huku akimtaka Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo pamoja na viongozi wengine wa Muleba kuendelea kuwatumia vijana hao katika kujenga miundombinu mingine kwani tayari wameonesha utayari na uwezo wa kufanya kazi hiyo kwa moyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news