Kenya yakabiliwa na ubaba wa kondomu

NAIROBI-Vituo kadhaa vya afya vya umma, hoteli na migahawa nchini Kenya vinakabiliwa na uhaba wa kondomu kutokana na mvutano wa ushuru kati ya wafadhili na serikali ya Kenya.
Kwa mujibu wa Gazeti la Daily Nation, mpango ambao hutoa kondomu za bure, sehemu muhimu ya kampeni ya Kenya ya kukabiliana na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwa( VVU), inategemea usaidizi wa wafadhili kununua bidhaa hizo.

Serikali ya Kenya husambaza bure karibu mipira milioni 180 kila mwaka kupitia mpango ambao unaofadhiliwa na Hazina ya Kimataifa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA)

Hata hivyo katika kipindi cha miezi mitatu iliyopiti, wagonjwa walio na virusi vya HIV katika makundi tofauti yamekuwa yakilalamikia uhaba wa kondomu nchini.

Mkurugenzi wa AIDS Healthcare Foundation amenukuliwa na Gazeti la Daily Nation akisema, mwaka huu serikali haikununua kondomu na shehena inayosambazwa na wakfu huo kwa sasa iliwasili nchini mwaka 2019.

Post a Comment

0 Comments