Kocha Kim Poulsen ataja kikosi cha Taifa Stars kitakachocheza mchezo wa Kufuzu Kombe la Dunia

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Ramadhani Suleiman Chombo (Redondo) amerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuelekea mchezo wa Kundi J kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Novemba 11,2021 katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam.

Mkongwe huyo katika soka ni miongoni mwa wachezaji 27 ambao wanaunda kikosi ambacho kimetajwa na kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mdenmark Kim Poulsen.
Aidha, kikosi hicho kinaundwa na makipa; Aishi Manula (Simba SC), Metacha Mnata (Polisi Tanzania), Ramadhani Kabwili (Yanga SC).

Mabeki ni Shomari Kapombe (Simba SC), Kibwana Shomari (Yanga SC), Israel Mwenda (Simba SC), Mohamed Hussein (Simba SC), Erasto Nyoni (Simba SC), Dickson Job (Yanga SC), Bakari Mwamnyeto (Yanga SC), Kennedy Juma (Simba SC), Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Edward Manyama (Azam FC), Nickson Kibabage (KMC FC).

Viungo ni Meshack Mwamita (Kagera Sugar FC), Novatus Dismass (Maccabi Tel Aviv), Muzamil Yassin (Simba SC), Ramadhani Chombo (Biashara United), Zawadi Mauya (Yanga SC), Feisal Salum (Yanga SC).

Pia washambuliaji ni John Bocco (Simba SC), Iddi Suleman (Azam FC), Abdul Suleiman (Coastal Union), Kibu Dennis (Simba SC), Reliant Lusajo (Namungo FC), Simon Msuva (Wydad AC) na Mbwana samatta (Royal Antwerp).

Post a Comment

0 Comments