MB Dogg afunguka mambo mazito kuhusu Diamond Platinumz na Harmonize

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MBWANA Mohammed Ali ambaye ni maarufu zaidi kwa jina lake la kisanii kama MB Dogg nchini huku akiwa amebobea katika muziki wa R&B na Bongo Flava ameamua kujitosa kimya kimya katika mvutano uliopo baina ya CEO wa Wasafi Classic Baby (WCB), Diamond Platinum na CEO wa Konde Music Worldwide, Harmonize.
MB Dogg ambaye ametamba katika tasnia hiyo tangu mwaka 2000 hadi leo huku akipata umaarufu zaidi kutokana na vibao vya Latifah, Waja, Mapenzi Kitu Gani, Inamaana na Natamani katika andiko lake mfululizo kupitia ukurasa wake wa Instagram anaonyesha kuguswa na mvutano unaoendelea baina ya mastaa hao wawili wa muziki nchini. Ufuatao ni mfululizo wa maandiko yake yanayohusiana na wasanii hao, endelea hapa chini....


SEHEMU YA 1

POLE RAJABU ABDUL KAHALI (KONDEBOY) MIKATABA (MAKUBALIANO).. CONTRACT 360 si mkataba mbaya kama unaelewa biashara ya muziki.

Ukielewa terms na condition (vigezo na masharti) unatoboa.But  (lakini) kwa mawazo yangu si mkataba mzuri kwa msanii underground (anayechipukia) ambae anaanza kuchipukia kupata nafasi na jina.

Kwanza anakuwa hajakomaa kimuziki na hayuko tayari kupokea umaarufu na kuweza kujiongoza kwenye uhalisia wa kupambana na MAISHA.

NITAJITOLEA MFANO MIMI BINAFSI NILIANZA SAFARI YANGU YA MUZIKI MIAKA YA 2000 kwenda 2003 rasmi.

Lakini nilipata umaarufu mkubwa nikiwa mdogo sana miaka 18 kwenda 20 ukomavu wangu kwenye biashara ya muziki na uelewa wangu ulikuwa mdogo sana, hasa kujiongoza kuweza kubalance maisha binafsi na muziki pia umaarufu na watu walionizunguka. 

Ilihitajika busara sana na uelewa mkubwa sana wa viongozi wangu ambao walinizunguka hasa msimamizi wa kampuni yetu kuniongoza kipindi hicho ambae kwa utendaji alikuwa Babu Tale, nilikuwa sijui chochote kuhusu kutunza pesa wala kutumia pesa.

Nyimbo yangu ya kwanza LATIFA ndio ilikuwa chanzo kikuu cha mapato kwenye kampuni badala ya mimi kufanikiwa kurekodi kwa gharama za boss (tajiri) wangu RIP (kwa sasa marehemu) my boss ABDUL.

Ulinipa kila kitu bila maandishi ya aina yeyote, Mungu akulaze pema BONGE.

Nilipata sifa zote kupitia roho yako na upendo wako kwa watu wote waliokuzunguka.

Uliwaamini watu ambao pia walikuja kukuangusha na kutuangusha tuliokuzunguka na kuanza kutapatapa ninaamini ungekuepo mpaka leo usingekubali kuona mimi nashindwa kwa njia yeyote ile.

UNAYOPITIA KONDE MIMI NILISHAPITIA KUANZIA MIAKA YA 2007 MPAKA HIVI SASA 2021.

NILIPOAMUA KUONDOKA KWENYE KAMPUNI ABDUL ALINIPA BARAKA, LAKINI HAKUWA NA FURAHA, SIKUELEWA SABABU NI NINI HASA.

LAKINI NILIANZA KUJUA BAADA YA KUTOA NGOMA YANGU YA KWANZA MWAKA 2008 INAYOITWA NATAMANI.

PESA ZILITOKA KUZUIA HII NYIMBO ISICHEZWE MEDIA (VYOMBO VYA HABARI) ZOTE NA KIPINDI HICHO HAKUNA DIGITAL PLATFORMS YEYOTE HAPA BONGO.

NILIPAMBANA KUVUKA MIPAKA HATIMAE NGOMA IKARUDI BONGO NA KUNIPA HESHIMA YA MSANII BORA WA KIUME MWAKA 2009/2010..

VIJANA SASA HIVI MNA NAFASI NYINGI UKIBANIWA RADIO UNAKWENDA YOUTUBE.

SISI KIPINDI CHETU HAKUNA HIZO MITANDAO. KWA HIYO HAYA MAMBO YALIANZIA MBALI TOKA ENZI ZETU. BAADA YA KUTOA NGOMA MILANGO YA SHOW IKAANZA.


SEHEMU YA 2


MILANGO YA SHOW IKAANZA KUFUNGUKA..HAPA NDIO BALAA LILIANZA KUNA BUSARA NILIITUMIA KIPINDI HICHO AMBAYO PIA ILINICOST (ILINIGHARIMU) SANA SIKUWAHI KUTANGAZA KAMA NILIKUWA NIMEACHANA NA MANEJIMENTI YANGU YA AWALI KUEPUSHA MALUMBANO KWENYE MEDIA.

KWA HIYO DEAL ZANGU ZOTE ZIKAWA ZINAPITIA CHINI YA MSIMAMIZI WANGU WA AWALI BABU TALE.

MIMI NILISHAWAHI KUZUZISHWA NIMEKUFA,NIMEACHA MUZIKI NA PIA NIMEKUWA CHIZI.

KWA KIFUPI SIKO TENA KWENYE GAME ILINIUMA SANA.

SHOW ZOTE ZILIZOKUWA ZINATOKA NJE ZILIZIMWA KWA SABABU ZILIKUWA ZINAPITIA HUKO SASA NAJARIBU KUELEZA WAKATI SISI VIJANA TUNAANZA MUZIKI HUWA HATUANGALII BIASHARA WALA PESA 

HUWA TUNAANGALIA SIFA NA MAPENZI YA DHATI YA MUZIKI SO JUKUMU LINABAKI KWA WAKUBWA ZETU AMBAO WAMETUSHIKA MKONO KUTUELEKEZA KUHUSU BIASHARA NA UMAARUFU.

SUALA LA MKATABA NI MUHIMU SANA KUMPA ELIMU KIJANA KABLA HAJASAINI NA PIA KUMSHAURI AWASHIRIKISHE WATU WENGINE TOFAUTI NA WAHUSIKA AMBAO NI VIONGOZI WAKE UMRI WA MIAKA 18 KIBONGO KUJUA CONDITION NA TERMS ZA MIKATABA NI NGUMU SANA.

PIA HAIWEZEKANI MWANASHERIA WA KAMPUNI HUSIKA NDIO AWE MTU WA MWISHO KUKUTOLEA MAAMUZI YA KUSAINI 

YAPASWA MKATABA PIA USHIRIKISHE MTAALAMU NJE YA KAMPUNI, TATIZO WANAOTOA MIKATABA WANATUMIA UDHAIFU NA UELEWA WA KIJANA KIPINDI HICHO INAKUWA KAMA MTEGO HII NI NOMA.

HAPA LENGO INAKUWA SIO KUENDELEZA KIPAJI NI KUUA KIPAJI.

VIJANA SISI NI WAGUMU KUELEWA NA KUSOMA MIKATABA BUT ANAEKUONGOZA YAPASWA AWE ANAJUA KUHUSIANA NA MIKATABA.

HARMONIZE INATEGEMEA JE ALIPEWA NAFASI YA KUSHIRIKISHA WASHAURI NJE YA WASAFI CLASSIC BABY NA PIA ALITAKIWA AWE NA MWANASHERIA WAKE BINAFSI TOFAUTI NA LABEL YAKE.

SASA UKIWA BADO MDOGO HIVI VITU HUWEZI KUVIJUA WANAOTAKIWA KUKUSHAURI NI HAO VIONGOZI WAKO.

SASA MTU ANAYEKUPA MKATABA KUKUPA USHAURI NI NGUMU NA WEWE UKIANGALIA UNATAMANI KUJULIKANA NA UPATE NAFASI UNAONA UNAPOTEZA MUDA UNAWEKA WINO TU.

HAYA NI MAKOSA SANA KWETU WASANII NOW IMEFIKA WAKATI WA KUBADILIKA SISI WENYEWE NA VIONGOZI AU WAWEKEZAJI, JUA VIJANA WOTE HATUNA ELIMU YA BIASHARA YA MUZIKI MUHIMU KUWASAIDIA VIJANA NA KUWAPITISHA KWENYE NJIA NZURI YA KUPAMABANA NA UMAARUFU.

KUVAA VIATU VYA DIAMOND PLATINUMZ au HARMONIZE KWA SASA NI KAZI NGUMU MIMI NIMEPITIA UMAHARUFU HUO NA USIPOPATA WASHAURI WAZURI UNAPOTEA


SEHEMU YA 3

HII BADO NI FAMILIA BORA SANA KWANGU KWA WAKATI WOTE.

MATATIZO YAPO NA YANASABABISHWA NA SISI BINADAMU KWA KUKOSA UELEWA.

NILIPOACHANA NA FAMILIA HII MOJA YA VIONGOZI WANGU ALIHAIDI NA KUHAKIKISHA KAMA WAO NDIO WALINITOA BASI NISUBIRI MAUMIVU KWENYE SAFARI YANGU YA MUZIKI NA KWA SABABU NILIKUWA SINA KIPATO CHOCHOTE CHA MOTO NIMEKIPATA MPAKA SASA WAMESHIKILIA HAKI ZANGU KWA NJIA ZA PANYA ILA HILI LITAKWISHA NA LITAWAGHARIMU WASIPOKUWA MAKINI.

KWENYE HILI LA KONDE HATUPASWI KUMLAUMU SANA DIAMOND PLATINUMZ WALA KULAUMIWA HARMONIZE.

HAWA VIJANA HAWANA WANALOLIFAHAMU KUHUSU KIWANDA CHA MUZIKI.NYUMA YAO KUNA WATU NI VIONGOZI.

KUMBUKA HAWA VIONGOZI WANA MAKOVU NA MAJERAHA AMBAYO KUPONA KWAKE NI KUFELI KWA DHAHABU AMBAZO WALIZICHIMBA MUDA MREFU NA ZIKAWATOKA MIKONONI.

TIPTOP CONNECTION, TMK WANUME FAMILY,BONGO RECORD,YAMOTO BAND,WAKALI KWANZA NA MAKUNDI MENGINE.

HAWA WATU HAWAWEZI KUONA WANASHINDWA KWA LOLOTE,MIMI NILIPENDEKEZWA KUINGIA KWENYE TUZO ZA MTV Africa Music Awards 2009.

Were held on October 10, 2009 at the gymnasium of the Moi International Sports Centre complex in Nairobi. 

HII DILI ILIIKUJA KUNIFIKIA MILANGO NDIO INAFUNGWA KWA SABABU NILITAKIWA KUWASILISHA WASIFU WANGU, LAKINI KWA SABABU LILIPITA KWA MTU AMBAE ALIKUWA MSIMAMIZI WANGU AMBAE ALIPATA UMAARUFU KUPITIA MIMI MPAKA AKAWA HAPO ALIPO AKAIMINYIA NDANI. 

SO NINACHOWEZA KUSEMA MFUMO WETU WA KIWANDA CHA MUZIKI HASA TANZANIA UNA MATATIZO MAKUBWA.

SERIKALI YAPASWA KUINGILIA KATI MATATIZO KAMA HAYA YAKO DUNIANI KOTE, LAKINI WENZETU SHERIA HUWA ZINAFUATA MKONDO WAKE WATU HAWATHUBUTU KUCHEZEA VIPAJI VYA WATU NAMNA HII.

TUMPONGEZE NASSIBU JAPO ANATUMIKA VIBAYA. KWA ANACHOKIFANYA KWANI KINALETA CHACHU NA SOLUTION YA HAYA YOTE.

NINA MENGI SANA SIKU NIKIRUHUSIWA KUONGEA NA VYOMBO VYA HABARI NITAYAWEKA WAZI NILIOWAKWAZA TUSAMEHEANE KWA HILI GAZETI.
Mvutano kati ya Harmonize na Diamond ulianza Agosti 8, 2019 pale mmoja wa Mameneja wa WCB, Mkubwa Fella alipochapisha ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram akieleza kuwa kuna watu wanamrubuni Harmonize kwa fedha ili aondoke kwenye lebo hiyo.

“Msiwarubuni vijana kwa pesa zenu, mnawafelisha, sisi ndio tupo mtaani tunajua maisha yao. Haya naona wengine mnaanza kumtia tamaa mwanangu Konde Boy, ila mwanangu ukiona ulipo inatosha sawa aga vizuri maana najua wenye hela za mjini wanapenda kugusanisha waya,” aliandika Mkubwa Fella.

Siku kadhaa mbele, aliyekuwa Meneja wa Harmonize, Mr Puaz akizungumza na BBC Swahili Agosti 25, 2019, alisema msanii huyo alikuwa na kiburi tangu aanze kupata mafanikio.

“Naelewa kwamba ni kijana mdogo ambaye ametoka katika familia masikini, lakini utajiri na umaarufu alioupata kutokana na mafanikio ya muziki wake umeathiri tabia yake,” alieleza.

Katika mahojiano yake, Harmonize alikana vikali madai kuwa Jembe ni Jembe ndiye alimshawishi kuondoka WCB Wasafi.

“Inaniumiza sana watu wanapoiweka kuwa Jembe ni Jembe ndio sababu ya mimi kuondoka WCB. Lakini naelewa sisi ni binadamu na kitu ambacho hukifahamu kiundani utakihukumu tu kwa namna unavyojua,” anasema Harmonize.

Akiwa kwenye jukwaa la Wasafi Festival mwaka 2019, Diamond Platnumz alieleza kwa hisia kali kusalitiwa na mtu wake wa karibuni aitwaye Jeshi. Huyu alikuwa ni Harmonize ambaye kwa wakati huo ndio tetesi za yeye kujitoa WCB Wasafi zilikuwa zimeshika kasi kwenye mitandao.

Tuhuma zote hizo kazijibu Harmonize hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa Instagram pamoja na mahojiano na Wanahabari Airport akitokea Marekani.

"Vijana ni vyema kujifunza ukimsaidia mtu sio lazima umdai fadhila maana kama ndio hivyo basi Tanzania yote inanidai pia," alisema Harmonize.

Post a Comment

0 Comments