Mgao wa fedha za UVIKO-19 waendelea kujenga madarasa kwa kasi Magomeni

NA ANNETH KAGENDA

FEDHA zilizotolewa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kupitia Mpango wa Serikali ya Tanzania wa Kuinua Uchumi kwa kutumia mkopo wa shilingi Trilioni 1.3 uliotolewa na Shirika la Fedha Duniani (IMF) ambazo kwa bahati nzuri Sekondari ya Magomeni imepata mgao wa kujengewa madarasa matatu, ujenzi huo unaenda kwa kasi na unatarajia kumalizika Desemba 15, mwaka huu.
Akizungumza na DIRAMAKINI Blog jijini Dar es Salaam akiwa eneo la ujenzi wa madarasa hayo (site), Diwani wa Kata ya Magomeni, Noordin Butembo amesema kuwa, zoezi linaenda vizuri.

Amesema, ujenzi huo unatarajia kukamilika mapema Desemba 15,2021 kutokana na kwamba fedha ya kufanya kazi hiyo ipo.

"Nimekuja kuangalia ujenzi unavyoendelea kutokana na kwamba tayari fedha ipo na kazi inabidi iendelee na ikamilike kwa wakati," amesema Diwani Butembo.

Aidha, amesema ujenzi wa madarasa hayo mara baada ya kukamilika utatumiwa na wanafunzi wa sekondari utasaidia kuondoa usumbufu kwani matatizo ya madarasa yatakuwa yamekwisha.

Pia alisema kutokana na uwepo wa madarasa hayo msongamano madarasani utapungua kama siyo kuisha kabisa.

Hata hivyo, Diwani Butembo alisema kuwa mara baada ya zoezi hilo kumalizika pia kuna zoezi la madarasa sita ya ghorofa yanaendelea na pia kuna maabara zinaendelea kujengwa.

Mmoja wa wananchi Fatuma Unji amesema, kuwepo kwa ongezeko wa madarasa hayo kutaongeza ufaulu kwani watoto watakaa kwa kujinafasi madarasani na kumsikiliza mwalimu kwa ufasaha.

"Kwenye kuboresha ni vyema viongozi wakajadiliana ili kutengeneza eneo la walimu kuwafundisha wanafunzi (hall) mara baada ya masomo wanabaki shule kusoma ambapo mzazi anakuwa hana wasiwasi na mtoto wake ni sehemu gani alipo kuliko kuzunguka kwenye nyumba za watu kutafuta walimu," amesema Dada Unji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news