Mwaka Mmoja wa Uongozi wa Rais Dkt.Mwinyi: Mbio za Uchumi wa Buluu zawaunganisha wengi

NA MWANDISHI MAALUM

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezindua mbizo za Zanzibar Blue Economy Half Marathon 2021 ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya sherehe za mwaka mmoja tokea ashike madaraka ya kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambapo leo yamefikia kilele.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika viwanja vya Mapinduzi Square Michezani kwa ajili ya kuaza kwa Mbio Zanzibar Blue Economoy Half Marathon 2021 za Kilomita 4 na kumalizia katika uwanja wa Amaan na kushoto kwa Rais ni Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na kulia kwa Rais ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, wakijiandaa kuaza mbio hizo zilizofanyika Novemba 6,2021 ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Mwaka Mmoja wa uongozi wake.(Picha na Ikulu).

Uzinduzi huo wa mbio hizo umefanyika leo Novemba 6, 2021 mapema saa 12 za asububi kwa kuanza kutimua vumbi katika eneo la Mapinduzi Square Mwembe Kisonge jijini Zanzibar na kuishia katika uwanja wa Amaan kwa kupitia katika mzunguko wa maeneo mbalimbali yaliyopangwa ambapo wanariadha hao walianza mbio hizo wakiwemo wakimbiaji wa kilomita 10 na wale wa kilomita 21.

Mara baada ya uzinduzi huo Rais Dkt.Mwinyi akiwa na Mama Maria Mwinyi aliwaongoza viongozi akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, wananchi pamoja na vikundi mbali mbali vya mazoezi katika matembezi ya kilomita nne yaliyoanza hapo Mapinduzi Square Mwembe Kisonge hadi uwanja wa Amaan, Jijini Zanzibar.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi alitoa vyeti kwa baadhi ya wadhamini wa mashindano hayo kwa niaba ya wenzao pamoja na kutoa kuwavisha nishani washindi wa mashindano hayo ambapo pia, alipata fursa ya kuangalia mashindano ya riadha ya wazee kuanzia miaka 60 pamoja na mashindano ya riadha kwa watu wenye ulemavu wa miguu. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika matembezi ya Marathon ya Kilomita 4, yalioazia katika eneo la Mapinduzi Square Michezani na kumalizia katika Uwanja wa Amaan Zanzibar na (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Mustafa Idrisa Kitwana na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, wakishiriki katika matembezi hayo ya Zanzibar Blue Economy Half Marathon 2021.(Picha na Ikulu).

Akitoa maelezo mafupi juu ya mashindano hayo, Mwenyekiti wa Zanzibar Blue Economy Half Marathon 2021, Abdalla Idrissa Majura alieleza kwamba mashindano hayo ni kwa ajili ya kumpongeza Rais Dk. Mwinyi kutimiza mwaka mmoja tokea aingie madarakani kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Majura alisema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya kuonekana kwamba Rais Dk. Mwinyi ameanza kutekeleza ahadi zake kwa vitendo akiwa na lengo la kuiletea maendeleo Zanzibar ambapo na wao wakiwa wanamichezo wanamuunga mkono Rais Dk. Mwinyi katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya (CCM).

Aidha, Mwenyekiti huyo alisema kuwa mashindano hayo pia, yanawasaidia wananchi wa Wazanzibari katika kufanya mazoezi kwa lengo la kupambana na maradhi yasioambukiza.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimvisha Nishani Mshindi wa kwanza wa Mbio za Kilomita 21 za Zanzibar Blue Economy Hafl Maradhon 2021 Francis Daman baada ya kubuka mshindi wa mbio hizo, zilizoazia katika eneo la Mapindizi Square Michezani na kumalizia Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu). Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasalimia Wananchi wakati akiwa katika Matembezi ya Kilimota 4 ya Zanzibar Blue Economy Hafl Marathon 2021 yaliyoazia katika eneo la Mapinduzi Square Michezani Jijini Zanzibar na kumalizia katika Uwanja wa Amaan na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi.(Picha na Ikulu).

Mwenyekiti huyo aliitaja mikakati waliyoiweka katika maandalizi ya mashindano hayo pamoja na namna ya upatikanaji wa fedha za mashindano hayo ulivyofanyika na kusisitiza haja ya mashindano hayo hapo mwakani kuungwa mkono zaidi na Serikali ili yawe ya Kimataifa kama yalivyo mashindano mengine yakiwemo yale ya Kilimanjaro Marathon.

Alieleza jinsi wadhamini mbali mbali waliojitokeza kuunga mkono mashindano hayo ya riadha ambapo miongoni mwa wafadhili hao ni Benki ya National Microfinance Bank (NMB) waliodhamini mashindano ya kilomita 21 ambapo mshindi wa mwanzo alikabidhiwa TZS milioni moja, mshindi wa pili laki 8 na wa tatu laki 5.

Pamoja na hayo, kwa upande wa mashindano ya killomita 10, kwa maelezo ya Mwenyekiti huyio Benki ya Kenya Commercial Bank (KBC) iliyadhamini ambapo mshindi wa kwanza alipata TZS laki 8, mshindi wa pili laki 5 na wa tatu alipata laki 3. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi Maalum ya picha yake ya kuchora iliotolewa na Kamati ya Maandalizi ya Zanzibar Blue Ecenomy Hafla Marathon 2021 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ndg Abdalla Majura, baada ya kumaliza Matembezi ya Kilomita 4 ya Zanzibar Blue Economy Hafl Marathon 2021.(Picha na Ikulu). Wananchi wakiwa katika barabara ya Amani wakimshangilia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akipita katika eneo hilo wakati akiwa katika Matembezi ya Kilomita 4 ya Zanzibar Blue Economy Hafl Marathon, ikiwa ni Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Uongozi wake.(Picha na Ikulu).

Pia, (KCB) wamedhamini mbio fupi za uwanjani ambapo wanariadha wastaafu kila mmoja atapata sh. 100,000 kwa wanaume na wanawake huku wanariadha wote 200 watakaoshiriki watapa 50,000 bila kujali mshindi wa mwanzo au wa mwisho.

Sambamba na hayo, Mwenyekiti huyo alisisitiza lengo la Kamati ya mashindano hayo la kusaidia ujenzi wa Soko la Fumba.

Wadhamini wengine wa waliosaidia mashindano hayo ni Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mohamed Raza kupitia ZAT, TRA, BUMACO POSTA,World of Sports Kikwajuni, PSSSF Zanzibar, Azam Media,TTCL, Shirika la Bandari Zanzibar pamoja na Sea Cliff Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news