Rais Dkt.Mwinyi akirejea nchini


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana Balozi wa Tanzania Nchini Afrika Kusini Meja Jenerali (Mst) Gaudance Milanzi na (kushoto kwake) Kiongozi wa Juu wa Serikali ya Afrika Kusini, Mhe.Mashego Dlamini na ( kulia kwake) Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Edwin Lutageruka, wakati akiondoa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Shaka jijini Durban Afrika Kusini leo Novemba 16,2021. akirejea nchini Tanzania.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na kuagana na Balozi wa Tanzania Nchini Afrika Kusini,Mhe. Meja Jenerali (Mst) Gaudance Milanzi na Kiongozi wa Juu wa Serikali ya Afrika Kusini Mhe. Mashego Dlamini, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Shaka Darban Jijini Afrika Kusini, baada ya kumalizika kwa mkutano wa Ufunguzi wa Maonesho ya Biashara kwa Nchi za Afrika uliofanyika katika ukumbi wa ICC Durban.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa na mwenyeji wake Kiongozi wa juu wa Serikali ya Afrika Kusini Mhe. Mashego Dlamini, akikagua gwaride maalum aliloandaliwa wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Shaka Jijini Darban Afrika Kusini leo 16-11-2021, akirejea Nchini Tanzania baada ya kumalizika kwa mkutano wa Ufunguzi wa Maonesho ya Biashara kwa Nchi za Afrika, uliofanyika katika ukumbi wa ICC Durban.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments