Rais Samia atuma salamu za pole kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Waziri wizara mbalimbali Mzee Al Noor Kassum

NA MWANDISHI MAALUM

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa pole Watanzania, wanafamilia kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri wa Fedha na Utawala wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Waziri Mstaafu wa Wizara tofauti kwenye Serikali ya awamu ya kwanza na pili, Al noor Kassum.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Salim Kassum ambaye ni Mtoto wa marehemu Al noor Kassum (wa pili kulia) na Muwakilishi Mkazi wa Taasisi ya Agha Khan nchini Tanzania Amin Kurji wakati alipomuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuaga mwili wa aliyekua Waziri wa Fedha na Utawala wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na aliyekua Waziri Mstaafu wa Wizara tofauti kwenye serikali ya awamu ya kwanza na ya pili, Al noor Kassum, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.

“Rais Mheshimiwa Samia amenituma niwape pole ndugu, familia na wote walioguswa na kifo cha Mzee Al noor Kassum. Mzee Kassum amefanya mambo makubwa sana kwenye nchi hii. Ametumikia Taifa kwa weledi, uaminifu na uadilifu mkubwa, Watanzania hatuwezi kumsahau.

Salamu hizo za pole zimetolewa leo Novemba 20, 2021 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Samia katika kuaga mwili wa Marehemu Kassum kwenye viwanja vya Karimjee mkoani Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ametoa wito kwa watumishi wa umma kuyaendeleza yote mazuri aliyoyafanya wakati wa utumishi wake ili Taifa liendelee kushamiri kwa maendeleo na amani. “Tuliokuwepo kwenye madaraka tuendeleze utawala unaojali wananchi kama alivyokuwa akifanya marehemu.”
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na waombolezaji wakati alipomuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuaga mwili wa aliyekua Waziri wa Fedha na Utawala wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na aliyekua Waziri Mstaafu wa Wizara tofauti wa serikali ya awamu ya kwanza na ya pili, Al noor Kassum, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akishiriki katika dua wakati alipoongoza waombolezaji kuaga mwili wa aliyekua Waziri wa Fedha na Utawala wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Waziri Mstaafu wa Wizara tofauti kwenye serikali ya awamu ya kwanza na ya pili, Al noor Kassum, kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.

Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwasihi Watanzania kila mmoja kwa imani yake waendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu Mzee Al noor Kassum.

Kwa upande wake, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema marehemu Mzee Kassum alimfundisha namna ya kufanyakazi na kuishi vizuri kati ya Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Waziri. Alimpokea wizarani alipoteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nishati, Maji na Madini wakati huo Mzee Kassum akiwa Waziri wa Wizara hiyo.

Naye, Waziri Mkuu Mstaaafu Cleopa David Msuya amesema marehemu Mzee Al noor Kassum popote alipopelekwa alifanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kuacha alama kwa mambo makubwa aliyolifanyia Taifa.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na waombolezaji wakati wa kuaga mwili wa aliyekua Waziri wa Fedha na Utawala wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Waziri Mstaafu wa Wizara tofauti kwenye serikali ya awamu ya kwanza na ya pili, Al noor Kassum, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiagana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kuwaongoza waombolezaji kuaga mwili wa aliyekua Waziri wa Fedha na Utawala wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na aliyekua Waziri Mstaafu wa Wizara tofauti kwenye serikali ya awamu ya kwanza na ya pili, Al noor Kassum, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba akizungumza na waombolezaji wakati wa kuaga mwili wa aliyekua Waziri wa Fedha na Utawala wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Waziri Mstaafu wa Wizara tofauti kwenye serikali ya awamu ya kwanza na ya pili, Mzee Al noor Kassum, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Sinde Warioba ambaye ametoa salamu za pole kwa niaba ya viongozi waliowahi kufanya kazi na marehemu Mzee Kassum amesema marehemu Mzee Al noor Kassum alijenga umoja wa kitaifa na alisimama katika kuondoa ubaguzi na alisisitiza amani na mshikamano.

Akisoma wasifu wa marehemu, Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato amesema marehemu Mzee Kassum alikuwa Waziri wa Nishati, Maji na Madini kati ya mwaka 1982 had mwaka 1988 na katika kipindi chake alisimamia mipango na utekelezaji wa miradi mbali mbali ya Nishati, Maji na Madini yenye manufaa makubwa kwa uchumi wa nchi.
Waziri Mkuu Mstaafu David Cleopa Msuya akizungumza na waombolezaji wakati wa kuaga mwili wa aliyekua Waziri wa Fedha na Utawala wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Waziri Mstaafu wa Wizara tofauti kwenye serikali ya awamu ya kwanza na ya pili, Mzee Al noor Kassum, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Novemba 20, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

“Katika Sekta ya Nishati, Mzee Kassum atakumbukwa kwa usimamizi wa ujenzi wa bwawa la kuhifadhi maji la Mtera lililochangia kuongeza uzalishaji umeme wa megawati 102 katika kituo cha Kidatu na megawati 80 katika kituo cha Mtera, hivyo kuingiza jumla ya Megawati 182 katika mfumo wa Gridi ya Taifa.”

Amesema katika kipindi chake cha uwaziri njia ya umeme ya msongo wa kilovolti 220 kutoka Kidatu hadi Morogoro na Morogoro hadi Dar es Salaam ilijengwa na kazi kubwa ya kupeleka umeme katika makao makuu ya mikoa yote ya Tanzania bara ilifanyika.

Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa katika sekta ndogo ya mafuta na gesi asilia, Mheshimiwa Kassum alitoa mchango mkubwa kwani ndipo kazi za utafiti wa mafuta na gesi asilia nchini zilipoanza chini ya Kampuni ya AGIP kwa kufanya utafiti katika maeneo mbalimbali likiwemo eneo la Mnazi Bay.

“Shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia zilishika kasi katika kipindi chake ambapo visima zaidi vilichimbwa katika maeneo ya Songosongo, Kimbiji na kina kirefu cha bahari. Jitihada zake zilichangia kwa kiasi Kikubwa ugunduzi na upatikanaji wa gesi tuliyo nayo nchini hivi sasa,"amesema.

Amesema wakati wa uongozi wake Kampuni ya TIPER ilianzishwa ili kuagiza mafuta ghafi ya jumla na kuyasafisha nchini na baadaye alisimamia mabadiliko ya sera ya mafuta yaliyoifanya TPDC kuwa mwagizaji wa jumla wa mafuta yaliyosafishwa na hivyo kuondoa tatizo kubwa la uhaba wa mafuta uliokuwepo wakati huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news