Serikali yawataka viongozi kusimamia kikamilifu ujenzi wa Sekondari ya Kwemkabala unaoigharimu TASAF milioni 66/-

NA VERONICA MWAFISI

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi amewaelekeza Viongozi wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, kuhakikisha wanasimamia kikamilifu ujenzi wa Shule ya Sekondari Kwemkabala unaogharimu shilingi milioni 66 zilizotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) baada ya kutoridhika na maendeleo ya ujenzi huo.
Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Kata ya Genge Wilaya ya Muheza jijini Tanga wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF na kuhimiza matumizi mazuri ya ruzuku inayotolewa na TASAF kwa walengwa.

Mhe. Ndejembi ametoa maelekezo hayo Novemba 24,2021 baada ya kukagua ujenzi wa shule hiyo akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Wilaya ya Muheza.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Kata ya Genge, Wilaya ya Muheza, jijini Tanga wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF na kuhimiza matumizi mazuri ya ruzuku inayotolewa na TASAF kwa walengwa.

Akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa Shule hiyo, Mhe Ndejembi amesema, kiasi cha fedha kilichotumika mpaka sasa hakiendani na kazi iliyofanyika na hii inatokana na ushauri au usimamizi mbaya uliotolewa juu ya ujenzi wa shule hiyo.

“Mhandisi anayesimamia ujenzi wa shule hii hakushauri vizuri kuanzia kwenye msingi mpaka ulipofikia, akiwa kama mtaalam, alitakiwa aangalie anachokishauri, kinachojengwa na thamani ya fedha iliyotolewa, hivyo Mkurugenzi na Watendaji wa TASAF muangalie namna gani ya kufanya ili jengo hili liweze kukamilika kwa ubora,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Mhe. Ndejembi ameongeza kuwa, kiasi cha fedha kilichobaki ambacho ni shilingi milioni 39 hakiwezi kukamilisha ujenzi wa shule hiyo kwa ubora kwani sehemu iliyobakia ni kubwa na fedha zilizobaki ni kidogo.
Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhe. Halima Bulembo, akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi kuzungumza na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Kata ya Genge, Wilaya ya Muheza, jijini Tanga wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Ndejembi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF na kuhimiza matumizi mazuri ya ruzuku inayotolewa na TASAF kwa walengwa.
Afisa Mtaalam wa Uwezeshaji, Ufuatiliaji na Ushauri kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Bw. Andrew Kibona akitoa ufafanuzi kuhusu Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kwa Walengwa wa Kata ya Genge, Wilayani Muheza wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Wilaya ya Muheza.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akitoa maelekezo baada ya kukagua ujenzi wa madarasa katika Shule ya Sekondari Kwemkabala Wilayani Muheza, jijini Tanga ambao unajengwa kwa kutumia fedha za TASAF wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Wilaya ya Muheza.

Mhe. Ndejembi amesema Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo, hivyo hafurahishwi kuona zikitumika vibaya.

Ujenzi wa shule hiyo unajumuisha vyumba viwili vya madarasa, ofisi na matundu matano ya vyoo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news