Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP Jeremiah Yoram Katungu, amewataka Maafisa Ustawi wa Jamii wa Jeshi la Magereza kuhakikisha wanawaelimisha wafungwa na mahabusu kuhusu haki na wajibu wao mara wanapopokelewa magerezani pamoja na taratibu zinazopaswa kufuatwa katika kipindi chote wanaposhikiliwa gerezani.
CGP Katungu ametoa maelekezo hayo Juni 12, 2026 wakati akifunga rasmi Mafunzo ya Maafisa Ustawi wa Jamii kuhusu Mwongozo wa Utekelezaji wa Programu za Urekebishaji yaliyofanyika kwa siku tatu katika Ukumbi wa Rugimbana, Msalato jijini Dodoma.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo





















