Simanzi zatawala watu waliofariki katika ajali ya moto

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Watu watano wa familia moja wamefariki dunia baada ya nyumba waliyokuwemo kuteketea kwa moto katika mtaa wa Mandela uliopo Igoma Mashariki jijini Mwanza.
Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji mkoani humo, Ambwene Mwakibete amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Mwakibete amesema kuwa moto huo umetokea usiku wa kuamkia Novemba 8, 2021.

"Ni kweli waliofariki ndani ni Lameck Benedicto, mke wake, mtoto wake wa kike na wageni wake wawili ambao bado majina yao hayajatambulika," amesema Mwakibete.


WATU WATANO (5) WA FAMILIA MOJA WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA AJALI YA MOTO KUUNGUZA NYUMBA, HUKO BARABARA YA TWIGA, MTAA WA IGOMA MASHARIKI, KATA YA IGOMA, WILAYA YA NYAMAGANA. WALIOFARIKI KATIKA AJALI HIYO YA MOTO NI LAMECK BENEDICTO, MIAKA 32, MSUKUMA, MWENDESHA BODABODA, MKAZI WA IGOMA, MKEWE AITWAYE LEYAH LAMECK, MIAKA 26, MKULIMA, MKAZI WA IGOMA MASHARIKI, MTOTO WAO YUNITH LAMECK, MWAKA 1, NA VIJANA WAWILI WAKIUME MAJINA YAO BADO KUFAHAMIKA AMBAO WALIMTEMBELEA TAREHE 07/11/2021.

TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 08/11/2021 MAJIRA YA SAA 00:05 USIKU MAENEO TAJWA HAPO JUU, HII NI BAADA YA NYUMBA NAMBA 21 MALI YA JAMASON SALUMU MBONABUCHA, MIAKA 41, MUHA, MFANYABIASHARA, MKAZI WA MBUGANI KATA YA KISHIRI, ILIYOJENGWA KWA TOFALI ZA SARUJI NA KUEZEKWA KWA BATI NA KUUNGANISHWA UMEME WA TANESCO IKIWA NA WAPANGAJI WANNE NDIPO CHUMBA NA SEBULE CHA MPANGAJI LAMECK BENEDICTO AMBAYE NI MAREHEMU KWA SASA GHAFLA KILIWAKA MOTO NA KUTEKETEA NA KUSABABISHA VIFO VYAO PAPO HAPO.

CHANZO CHA MOTO HUO BADO KINACHUNGUZWA, MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MKOA YA SEKOU- TOURE KUSUBIRI UCHUNGUZI WA DAKTARI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ITAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI. THAMANI YA MALI ZILIZOTEKETEA KATIKA AJALI HIYO BADO HAZIJAJULIKANA. JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LINAENDELEA NA UCHUNGUZI KUHUSIANA NA TUKIO HILO.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news