Simba SC yamtangaza aliyewahi kuwa kocha Real Madrid kuwa kocha mkuu

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Real Madrid ya Uhispania, Pablo Franco ametangazwa kuwa kocha mpya wa Simba SC ya Tanzania.
Simba imeingia mkataba wa miaka miwili na mwanasoka huyo wa zamani wa Uhispania.

Franco anachukua nafasi ya Didier Gomes raia wa Ufaransa ambaye mkataba wake ulisitishwa wiki mbili zilizopita baada ya makubaliano baina ya pande zote kufikiwa.

Aidha, kabla ya kujiunga Simba SC alikuwa kocha wa Al Qadsia ya Kuwait na amewahi kuwa kocha wa Getafe 2015.

Post a Comment

0 Comments