Taasisi ya Liwancy yawakutanisha wadau na kumpongeza Rais Samia

NA ANNETH KAGENDA

TAASISI ya Liwancy nchini Tanzania inayojishughulisha na kilimo cha mazao mbalimbali kubwa likiwa ni zao la korosho imekutana na wadau pamoja na waandishi wa habari, lengo likiwa ni kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wake wa kazi iliyotukuka.
Kadhalika, Mshauri wa Liwancy nchini, Charles Sabinian (Lowassa), ambaye pia ni Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amempongeza kwa dhati kwa utendaji kazi mzuri Rais Mama Samia na kusema kuwa awali alizuru Bagamoyo na kutembelea, ngome ya Kaole na kujionea mambo mbalimbali na kusema kuwa mwanamke alitabiriwa kwamba ataongaza miaka ijayo.

"Na kwa sasa utabiri huu umedhihirika kwamba Mama Samia ndiye anayeongoza nchi kwa sasa,".

Lowassa, kwenye kikao hicho alisema kuwa mama Samia amekuwa msaada mkubwa kwa vijana, kwani hata Wamachinga amewatafutia maeneo ya kufanya shughuli zao.

Aidha, amesema kuwa Rais pia amekuwa mstari wa mbele kuwatetea vijana wa kitanzania katika kuhakikisha wanajipatia kipato kutokana na kwamba anaenzi uongozi wa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt.John Pombe Joseph Magufuli.

Mshauri wa Liwancy, Lowassa, alisema kuwa Rais Samia amekuwa akifanya mambo makubwa ambayo hata kwa vijana yamekuwa yakileta tija kwa nchi.

Mwakilishi wa Liwancy ambaye ni Msaidizi wa Afisa Mtendaji Mkuu, George Solo amesema kuwa, mkutano huo ulikuwa kwa ajili ya kukutana na waandishi wa habari pamoja na wadau wa maendeleo ili kujadili maendeleo ya kampuni.

George amesema kuwa, lengo pia lilikuwa kumpongeza Mama Samia kwa utendaji wake wa kazi kubwa na uliotukuka ikiwemo kufuatilia mambo ya maendeleo ya vijana wa nchi yake.
Hata hivyo amesema kuwa, wana mpango wa kuajiri vijana wengi zaidi kwenye taasisi yake ili kuepukana na tatizo la umaskini nchini.

Mgeni mwalikwa Kijana Kiboko Manyerere Nyerere amesema kuwa, kikao hicho ni cha msingi na kwamba wanaiomba serikali kuunga mkono taasisi ya Liwancy kwani ipo kwa ajili ya kuwasaidia vijana na kumuunga mkono mama.

Manyerere amewaomba vijana kuchangamkia fursa na kuendelea kumuunga mkono mama Samia katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya nchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news