TANESCO kugeukia gesi asilia uzalishaji umeme

NA GODFREY NNKO

SHIRIKA la Umeme nchini (TANESCO) limesema linachukua hatua za haraka kwa kuongeza uzalishaji kwa kutumia gesi asilia.
Hatua hizo ni kutokana na mabadiliko ya hali hewa, kupungua kwa kiwango cha maji katika mito na mabwawa nchini.

Kwa mujinbu wa taarifa ya TANESCO iliyotolewa Novemba 18, 2021 imesema hali ya upungufu huo imeathiri uzalishaji katika vituo vya kuzalishia umeme vinavyotumia maji.

“Athari kubwa imetokea katika vituo vyetu vya Kihansi, Kidatu na Pangani. Jumla ya upungufu wa uzalishaji ni nakribani megawati 345 ambayo ni asilimia 21 ya uzalishaji wote,” imeeleza taarifa hiyo.

Aidha, shirika hilo limesema linachukua hatua za haraka kuongeza uzalishaji kwa kutumia gesi asilia kwa kuharakisha matengenezo ya baadhi ya mitambo yake ya Ubungo I inayozalisha Megawati 25.

Vituo vingine ni Kinyerezi I Megawati 185, Ubungo III Megawati 112, pamojqa na kuwasha kituo cha Nyakato kinachozalisha Megawati 36 hali itakayofanya kuwa na jumla ya megawati 358.

“Kwa kuwa kutakuwa na upungufu kwa baadhi ya mikoa taarifa zitatolewa kwa wakati ili wateja waweze kupanga kazi zao,”imeongeza taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news