Tanzania yang'ara COSAFA Beach Soccer 2021

NA MWANDISHI MAALUM

WATANZANIA wameendelea kuonyesha juhudi mbalimbali katika soka ambapo kwenye michuano ya Soka la Ufukweni wamemaliza wa pili.

Ni baada ya kufungwa 3-1 na Msumbiji katika Fainali za Ufukwe wa South Beach Arena mjini Durban, Afrika Kusini.
Ushindi huo ni mwendelezo wa ubabe wa Msumbiji kwa Tanzania, kwani mechi ya Kundi B walishinda kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 4-4.

Mechi nyingine Tanzania iliyo chini ya kocha Boniphace Pawasa ilishinda 3-1 dhidi ya Comoro Kundi A kabla ya kuifunga Angola 5-2 kwenye Nusu Fainali.

Post a Comment

0 Comments