Wavamizi wa Msitu wa Hifadhi ya Mgori watakiwa kuondoka mara moja

NA MWANDISHI MAALUM

WAVAMIZI wa msitu wa Hifadhi ya Mgori uliyopo mpakani mwa Wilaya ya Singida Vijijini na Mkoa wa Manyara wametakiwa kusitisha shughuli wanazoziendeleza ndani ya msitu huo na kuondoka mara moja katika eneo hilo kwa kuwa eneo hilo ni la uhifadhi.
Kauli hiyo imetolewa Novemba 18,2021 na Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dkt. Binilith Mahenge wakati wa majumuisho ya ziara yake kwenye msitu wa hifadhi hiyo ambayo alijionea uharibifu mkubwa iliyokuwa unaendelea ikiwa ni pamoja na ukataji wa miti, uhomaji wa mkaa na uanzishwaji wa makazi ndani ya hifadhi.
Katika ziara hiyo iliyokuwa na lengo la kutembelea na kujionea hali ya uharibifu katika hifadhi hiyo, walikuta maboma kadhaa yamejengwa na yanaishi watu na ukataji wa miti pamoja na uchomaji wa mkaa.

Akiwa katika hifadhi hiyo mkuu wa Mkoa ameshangazwa na kitendo cha wavamizi kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Manyara kuhamia msitu na kudai kwamba wameuziwa na wakazi wa maeneo hayo huku wengine wakidai wameruhusiwa na Serikali.

Kutokana na mkanganyiko huo Mkuu wa Mkoa akawataka kuondoka maeneo hayo ndani ya siku tatu huku akiitaka kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Singida na viongozi wengine kuandaa mkakati wa kuwaelimisha wananchi wa eneo hilo kuhusu athari ya uharibifu wa msitu huo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Binilith Mahenge akisisitiza jambo wakati wa ziara hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Paskas Muragili, akielezea jambo wakati wa ziara.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Vijijini, Mhe. Elia Digha akielezea jambo wakati wa ziara.

Aidha, Mkuu wa mkoa amebainisha kwamba Serikali ilikuwa na nia nzuri kuwaambia wananchi kuyatumia bĂ adhi ya maeneo lakini hawakutakiwa kutumia maeneo ya Hifadhi ya msitu.

Dkt. Mahenge akawataka Wakala wa Uhifadhi ya misitu Nchini (TFS) kuandaa mikakati ya haraka ya kunusuru msitu huo.

Post a Comment

0 Comments