Waziri Mkuu mgeni rasmi Mkutano wa Wadau wa lishe Tanga leo

NA HADIJA BAGASHA

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa wadau wa lishe utakaofanyika jijini Tanga leo Novemba 18, Mwaka huu wakiwemo mawaziri saba kutoka wizara mbalimbali ambao watashiri mkutano huo.

Mkutano huo pia utazindua mpango wa lishe awamu ya pili inayoanzia mwaka 2022 hadi mwaka 2026 na kubeba kauli mbiu isemayo lishe bora ni msingi wa maendeleo ya rasilimali watu katika uchumi shindani.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Tanga.

Amesema, mkutano huo unafanyika wakati kukiwa na tatizo la lishe nchini Tanzania na kueleza kuwa moja ya tatu ya watoto wa Tanzania wana udumavu jambo ambalo mkutano huo unaenda kuona kwa namna gani linakwisha.

"Lengo la kauli mbiu hiyo ni kuhakikisha watanzania wote wanaunga mkono juhudi za serikali katika kutekeleza mpango wa miaka mitano ya kuleta maendeleo ya kiuchumi katika Taifa, "amesititiza Waziri Mhagama.

Ameongeza kuwa suala la udumavu, utapiamlo wa muda mrefu wameweza kutoka asilimia 34.7 mwaka 2014 hadi kufikia asilimia 1.8 jambo ambalo limeleta matokeo makubwa.

Awali akizungumzia kuhusu mwanawake, Waziri Mhagama amesema moja ya tatu ya waliopo kwenye umri wa kuzaa wana upungufu wa damu tatizo linalosababishwa na lishe duni huku kwa upande wa watu wazima moja ya tatu yao wanatatizo la uzito uliozidi kiasi au kiribatumbo.

"Ukondefu kiwanda cha kitaifa kimeshuka kutoka asilimia 3.8 hadi asilimia 3.5 utoaji wa huduma za lishe katika utoaji wa huduma kwenye ngazi za jamii umeendelea kushuka, "amesisitiza Mhagama.

Jumla ya wadau 150 kutoka katika sekta mbalimbali watashiriki kwenye mkutano huo.

Post a Comment

0 Comments