Waziri Ndaki agoma kufungua kiwanda cha nyama ya punda

NA KADAMA MALUNDE

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki amekataa kufungua kiwanda cha Uchinjaji, Uchakataji na Usafirishaji wa nyama ya Punda cha Fang Hua Investment Co. Ltd kilichopo Ibadakuli mjini Shinyanga.

Ni kutokana na kushindwa kufuata masharti waliyopewa na wizara hiyo ikiwemo kuwa na mashamba ya kufugia punda na kuhimilisha punda ili kuongeza idadi ya punda wanaotakiwa kuchinjwa.
Muonekano wa shamba la kufugia punda katika kiwanda cha Uchinjaji, Uchakataji na Usafirishaji wa nyama ya Punda cha Fang Hua Investment Co. Ltd kilichopo Ibadakuli mjini Shinyanga. (Picha zote na Kadama Malunde).

Waziri Ndaki ametoa zuio hilo leo Jumanne Novemba 30,2021 alipotembelea kiwanda hicho cha Fang Hua Investment Co. Ltd kilichopo Ibadakuli mjini Shinyanga akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko pamoja na wataalamu mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo kutoka Wizara ya Ufugaji na Uvuvi, Prof.Hezron Nonga.

Waziri Ndaki amesema amefika katika kiwanda hicho kutokana na ombi la Wawekezaji hao kuomba Waziri afike kiwandani hapo kuangalia namna walivyochukua hatua za kuboresha mazingira ili waanze uzalishalishaji baada ya serikali kuagiza kiwanda hicho kisitishe uzalishaji mwezi Oktoba 2021 kutokana na mapungufu yaliyojitokeza.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki akizungumza leo Novemba 30, 2021 kwenye kiwanda cha Uchinjaji, Uchakataji na Usafirishaji wa nyama ya Punda cha Fang Hua Investment Co. Ltd kilichopo Ibadakuli mjini Shinyanga.

“Tulisitisha uzalishaji wa mazao kutokana na sababu ambazo mnazifahamu, baada ya kusitisha mmekaa baada ya mwezi mmoja mkaandika barua kwangu wizarani, mkiomba tuje tuangalie tuone kama yale masharti na vigezo mlivyopewa mmevikamilisha. Nyinyi mlisema mpo tayari kwa sababu masharti yale mmeshayakamilisha na kwa hiyo mkawa mnaomba mfunguliwe tena, muanze uzalishaji,"amesema Waziri Ndaki.

“Lakini nasikitika kuona hali halisi ya kiwanda chenu na vigezo na masharti ambayo mliambiwa bado hamjayakamilisha,mliambiwa muwe shamba la kufugia punda bado hamnayo,mnasema mnayo mmenunua shamba kule Kishapu, lakini lile shamba halina punda na lipo kwenye hatua za mwanzoni kabisa, lakini mliambiwa muwe na wafugaji wa punda wa mkataba ambao watahakikisha wanazalisha punda wa kuwauzia ili hawa punda kwa sababu ni wanyama adimu msije mkachinja mkawamaliza lakini bado hakuna wafugaji mliowapa mikataba na wanafanya hivyo,”ameeleza Waziri Ndaki.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha Fang Hua Investment Co. Ltd, Bw. Jiao Zhil Ing (kulia) wakati akiangalia shamba la kufugia punda katika kiwanda cha Uchinjaji, Uchakataji na Usafirishaji wa nyama ya Punda cha Fang Hua Investment Co. Ltd kilichopo Ibadakuli Mjini Shinyanga.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki (kushoto) akiangalia shamba la kufugia punda katika kiwanda cha Uchinjaji, Uchakataji na Usafirishaji wa nyama ya Punda cha Fang Hua Investment Co. Ltd kilichopo Ibadakuli Mjini Shinyanga. Shamba hilo lina punda 25.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki (kushoto) akiangalia shamba la kufugia punda katika kiwanda cha Uchinjaji, Uchakataji na Usafirishaji wa nyama ya Punda cha Fang Hua Investment Co. Ltd kilichopo Ibadakuli Mjini Shinyanga. Shamba hilo lina punda 25.

“La tatu nyinyi wenyewe mlisema kwamba punda ili waendelee kuwepo na kiwanda chenu kiendelee kufanya kazi tutapata punda kutoka China ambao mtawaleta ili mfanye kazi ya uhimilishaji, punda wazaliane wawepo kwa wingi na kiwanda chenu kipate malighafi kwa ajili ya kazi mnayoifanya, hamjaleta, hamjaanza kuhimilisha punda. Sasa mliposema tuwafungulie ni masharti yapi sasa mliyokamilisha, kwa sababu tulichokiona ni sasa mmeachana na kitendo cha kupiga punda nyundo na sasa mnatumia mashine,”ameongeza Waziri Ndaki.

Waziri huyo amefafanua kuwa, Serikali imetoa maelekezo ya namna ya kufanya biashara hiyo ya kuchinja punda kwa uendelevu bila kuathiri upatikanaji wa punda nchini na kutokana na kwamba hawajatimiza masharti hivyo hawezi kufungua kiwanda hicho.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki (katikati) akitoka katika shamba la kufugia punda katika kiwanda cha Uchinjaji, Uchakataji na Usafirishaji wa nyama ya Punda cha Fang Hua Investment Co. Ltd kilichopo Ibadakuli Mjini Shinyanga. Shamba hilo lina punda 25. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki (katikati) akitembelea kiwanda cha Uchinjaji, Uchakataji na Usafirishaji wa nyama ya Punda cha Fang Hua Investment Co. Ltd kilichopo Ibadakuli Mjini Shinyanga
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki (katikati) akitembelea kiwanda cha Uchinjaji, Uchakataji na Usafirishaji wa nyama ya Punda cha Fang Hua Investment Co. Ltd kilichopo Ibadakuli Mjini Shinyanga
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Utumishi wa kiwanda cha Uchinjaji, Uchakataji na Usafirishaji wa nyama ya Punda cha Fang Hua Investment Co. Ltd kilichopo Ibadakuli Mjini Shinyanga, Jipayi Daudi.

“Mimi nasikitika kusema kiwanda hiki bado hatuwezi kukifungua leo kwa sababu masharti bado hayajakamilishwa, fuateni utaratibu tulioelekezana, mkikamilisha tutakuja tuangalie. Timu yetu ya wataalamu imekuja hapa na kubaini kasoro nyingi sana ikiwemo kukosekana kwa mashamba ya kufugia punda, wafugaji wa punda wa mikataba na uwepo wa punda wachache sana ambapo punda walioonekana Kiwandani ni 25 tu. Kweli kabisa punda 25 tu mnafuga? Hatuwezi kuwa na utani wa namna hiyo,”amesema Waziri Ndaki.

Amesema, kutokana na kiwanda hicho kutotekeleza masharti hayo ikiwemo kuendelea kuwa na idadi ndogo ya punda na kama hawajachukua hatua hizo endapo serikali itaruhusu kiwanda kianze kufanya kazi, wanaweza kuchukua punda kutoka kwa wafugaji na kuhatarisha uwepo wa punda nchini kitu ambacho kinapigiwa kelele na mataifa mbalimbali Duniani.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza katika kiwanda cha Uchinjaji, Uchakataji na Usafirishaji wa nyama ya Punda cha Fang Hua Investment Co. Ltd kilichopo Ibadakuli Mjini Shinyanga.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki (kulia) akitembelea kiwanda cha Uchinjaji, Uchakataji na Usafirishaji wa nyama ya Punda cha Fang Hua Investment Co. Ltd kilichopo Ibadakuli Mjini Shinyanga
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki (kulia) akitembelea kiwanda cha Uchinjaji, Uchakataji na Usafirishaji wa nyama ya Punda cha Fang Hua Investment Co. Ltd kilichopo Ibadakuli Mjini Shinyanga.“Punda ni wanyama adimu hatuwezi kuruhusu punda wapotee.Bado idadi ya punda mlionao ambao ni 385 kutoka kwa wafugaji 57 haitoshi kuendesha shughuli za uzalishaji kiwandani”,amesema.

“Nguvu kubwa ya kuweka hapa ni nyinyi kuwa punda wa kutosha,mjitosheleze. Leo tulitamani kuona hapa mna shamba la kufugia punda, mnavuna tayari,mnawalisha, mnazalisha ama mnahimilisha punda.Timizeni masharti haya, tuko tayari kufanya kazi pamoja na nyinyi.Lakini msipotimiza lazima tufuate sheria na taratibu za nchi yetu,”amesema Ndaki.

Amewataka wawekezaji nchini kufuata sheria na kanuni na makubaliano mbalimbali yanayowekwa.
Muonekano wa maboksi 900 ya nyama ya punda katika chumba cha ubaridi (Cold room) yenye uzito wa kilo 25 kila mmoja sawa na jumla ya kilo 22,500 za nyama ya punda ambazo hazijasafirishwa tangu kusitishwa kwa uchinjaji wa punda cha Fang Hua Investment Co. Ltd mwezi Oktoba 2021.
Muonekano wa ngozi za punda katika kiwanda kwa uchinjaji wa punda cha Fang Hua Investment Co. Ltd.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki (kulia) akitembelea kiwanda cha Uchinjaji, Uchakataji na Usafirishaji wa nyama ya Punda cha Fang Hua Investment Co. Ltd kilichopo Ibadakuli Mjini Shinyanga.
Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Hezron Nonga akionesha kitu kwenye kiwanda cha Uchinjaji, Uchakataji na Usafirishaji wa nyama ya Punda cha Fang Hua Investment Co. Ltd kilichopo Ibadakuli Mjini Shinyanga.
Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Hezron Nonga akizungumza katika kiwanda cha Uchinjaji, Uchakataji na Usafirishaji wa nyama ya Punda cha Fang Hua Investment Co. Ltd kilichopo Ibadakuli Mjini Shinyanga.

Naye Meneja wa Kiwanda cha Fang Hua Investment Co. Ltd, Bw. Jiao Zhil Ing amesema kiwanda hicho kimeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha ikiwemo kuanzisha kwa mashamba mawili ya kufugia punda,kuwa na wafugaji 57 wa mkataba na kufanya kuwa na punda 385 hivyo kuiomba serikali kuruhusu kiwanda hicho kiendelee kufanya shughuli za uzalishaji wakati kikiendelea kuboresha zaidi mazingira ya uzalishaji.

Jiao Zhil Ing ameeleza kuwa, baada ya kusitishwa kwa uchinjaji wa punda katika kiwanda chao cha Fang Hua, kampuni yao imekuwa ikifanya juhudi nyingi kurekebisha mapungufu mbalimbali ili kuweza kuruhusiwa kuanza kuchinja punda tena ikiwa ni pamoja na kuanzisha mashamba ya kufugia punda,kutoa mafunzo kwa wafugaji kadhaa mkoani Shinyanga kama wafugaji wa mkataba.

“Tumeanzisha shamba la kufugia punda hapa kiwandani lenye ukubwa wa ekari 20, tumeweka uzio na maeneo yamelimwa na kupandwa malisho na kuboresha miundombinu kwa kuweka vibanda,kivuli na mabirika ya maji. Tuna punda 25 hapa kiwandani. Shamba la pili lenye ukubwa wa ekari 33 lipo katika halmashauri ya Kishapu”,amesema Jiao Zhil Ing.


Aidha amesema kiwanda hicho kina maboksi 900 ya nyama ya punda katika chumba cha ubaridi (Cold room) yenye uzito wa kilo 25 kila mmoja sawa na jumla ya kilo 22,500 za nyama ya punda ambazo hazijasafirishwa tangu kusitishwa kwa uchinjaji wa punda mwezo Oktoba 2021.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki akizungumza kwenye kiwanda cha Uchinjaji, Uchakataji na Usafirishaji wa nyama ya Punda cha Fang Hua Investment Co. Ltd kilichopo Ibadakuli Mjini Shinyanga.
Meneja wa Kiwanda cha Fang Hua Investment Co. Ltd, Bw. Jiao Zhil Ing akieleza namna kampuni yao imekuwa ikifanya juhudi nyingi kurekebisha mapungufu mbalimbali ili kuweza kuruhusiwa kuanza kuchinja punda tena ikiwa ni pamoja na kuanzisha mashamba ya kufugia punda,kutoa mafunzo kwa wafugaji kadhaa mkoani Shinyanga kama wafugaji wa mkataba.
Mkalimani wa kiwanda cha uchinjaji wa punda cha Fang Hua Investment Co. Ltd, Venance Mahe akielezea namna wanavyoendelea kuboresha mazingira ya uzalishaji katika kiwanda hicho ikiwemo kuanzisha mashamba ya kufugia punda.
Mfanyakazi wa Kiwanda cha uchinjaji wa punda cha Fang Hua Investment Co. Ltd,, Isack Luhumbika akiomba serikali kuruhusu kiwanda hicho kiendelee kufanya kazi wakati kikiendelea kufanya marekebisho kutokana na mapungufu yaliyojitokeza.
Mfanyakazi wa Kiwanda cha uchinjaji wa punda cha Fang Hua Investment Co. Ltd, Isack Luhumbika akiomba serikali kuruhusu kiwanda hicho kiendelee kufanya kazi wakati kikiendelea kufanya marekebisho kutokana na mapungufu yaliyojitokeza.

Kwa upande wake mmoja wa wafanyakazi wa Kiwanda hicho, Isack Luhumbika ameiomba serikali kuruhusu kiwanda hicho kiendelee kufanya kazi wakati kikiendelea kufanya marekebisho kutokana na mapungufu yaliyojitokeza.

“Mhe. Waziri nina ombi, Hii Kampuni imeshikilia ustawi wa watu wengi sana wanaoishi eneo hili. Pamoja na kwamba serikali imekuwa ikileta mapendekezo mbalimbali ya kuboresha, na kwa kweli wawekezaji hawa wameonesha nia na wameanza kutekeleza maagizo ya serikali ikiwemo kuanzisha mashamba ya kufugia punda hapa kiwandani na kule wilayani Kishapu,”amesema Luhumbika.

“Najua serikali inawapenda watu wake mojawapo ni sisi wafanyakazi wa kiwanda hiki.Sisi wafanyakazi sasa hatuna uhakika wa lini tutaanza kufanya kazi,tukiangalia punda waliopo ni wachache na uzalishaji ukisimama hatuwezi tena kufanya kazi, Ombi langu ni kwamba kwa sababu wawekezaji hawa wameshaonesha nia na wameanza kuchukua hatua maana yake wameiheshimu serikali, wametii mamlaka kwa kuanzisha mashamba ya kufugia punda tunaomba tuendelee na uzalishaji ili tuendelee kuwepo kiwandani kwa ustawi wetu. Wakiwa wanakamilisha masharti uzalishaji uendelee”,ameongeza Luhumbika.

Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Hezron Nonga amesema nchini Tanzania kuna uwepo wa idadi ndogo sana ya punda ambao wanakadiriwa kuwa chini ya 500,000 na kwamba mnyama punda ana faida nyingi kwa jamii hivyo ni vyema serikali ikafanya mikakati mbalimbali kuwatunza punda wachache waliopo ili waendelee kutumika kama wanyama kazi hasa katika maeneo ya vijijini.

Post a Comment

0 Comments