DC Msando afanya ziara ya kushtukiza kwenye vyanzo vya maji

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MKUU wa Wilaya ya Morogoro mkoani Morogoro, Mhe.Albert Msandoamefanya ziara ya kushtukiza katika Kata ya luhungo iliyopo Manispaa ya Morogoro kwa lengo la kukagua vyanzo vya maji.
Ziara hiyo ya Desemba 4,2021 pia iliangazia uharibifu wa mazingira unaofanywa na wananchi waishio pembezeno mwa vyanzo vya maji.
Pamoja na mambo mengine, Mheshimiwa Msando amezindua zoezi la upandaji miche ya miti ya aina mbalimbali katika eneo la Mtaa wa Mkoya Kata ya Luhungo pembezoni mwa Bwawa la Mindu.
DC Msando katika kuona zoezi hilo linakuwa na mafanikio,amewakutanisha viongozi wa taasisi za bonde la mto RUVU, TFS,MORUWASA pamoja na taasisi isiyokuwa ya kiserilaki ya RALEIGH Tanzania.

Aidha, amesema kuwa lengo la kuwakutanisha lilikuwa ni kuhamasisha jamii katika uhifadhi wa maji kwa kutumia misitu.
Pia DC Msando amempongeza Afisa Mtendaji wa Kata ya Luhungo, John Joseph kwa utayari wake wa kufanya kazi kubwa ya kuwatumikia wananchi wa kata hiyo ambapo aliahidi kumpa ushirikiano wa dhati katika kutunza na kuhifadhi vyanzo hivyo vya maji na kwamba zoezi hilo la doria liendelee bila kukoma na akamuahidi Mtendaji kumuongezea askari wengine zaidi ili waweze kufanya kazi kikamilifu.

Post a Comment

0 Comments