IGP Sirro awatumia salamu wahalifu wote nchini

NA GODFREY NNKO

MKUU wa Jeshi la Polisi mchini, IGP Simon Sirro amewaonya wanaojipanga kufanya uhalifu wa kutumia silaha katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka kwa kigezo cha kutafuta fedha, jambo ambalo halikubaliki na watambue kuwa, wapo macho muda wote.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akiwavalisha vyeo maofisa wapya sita waliofanya vizuri kati ya wahitimu 748 waliofanya Mafunzo ya Uofisa (Gazetted Officers) katika hafla ya ufungaji mafunzo iliyofanyika leo Desemba 12, 2021 katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam.

IGP Sirro ameyasema hayo leo Desemba 12, 2021 wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya askari wa jeshi hilo yaliyofanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam.

Tunapokaribia sikukuu za mwisho wa mwaka wale ambao silaha zao wamezifisha wanaamua kuingia barabarani kutafuta fedha. Niwaombe sana Watanzania tumalize mwaka vizuri, hauna sababu ya kuingia kwenye makosa haya ya bunduki unatisha Watanzania bila sababu na kujiweka maisha yako hatarini,”amesema IGP Sirro.

Pia amesema, kwa upande wa usalama nchini,hali ni shwari ingawa bado kuna matukio ya uhalifu ambayo wameendelea kuyadhibiti kila kona.

IGP Sirro amesema, wameweka mikakati kadhaa ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi, kushirikisha viongozi wa vijiji, mitaa, kata na shehia katika doria za mitaani na kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi ili kuweza kudhibiti vitendo hivyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news