Miaka 60 ya Uhuru: Tanzania yazidi kuwa mahali salama pa kuwekeza miradi mikubwa, Rais Samia azindua kiwanda kikubwa cha vifaa vya umeme

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Desemba 6, 2021 amezindua kiwanda cha kutengeneza vifaa vya umeme cha Elsewedy (Elsewedy Electric East Africa Ltd), kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Viongozi wakifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati akizindua rasmi Awamu ya Kwanza ya Kiwanda cha Vifaa vya Umeme cha Elsewedy Electric East Africa LTD kilichopo Kisarawe II Kigamboni jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Ikulu).

Ufunguzi wa Kiwanda hicho ni Sehemu ya maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru ambapo Mhe. Rais anaweka Mawe ya Msingi na kufungua miradi mbalimbali ya Maendeleo.

Mhe. Rais Samia amesema, uwekezaji wa Kiwanda hicho ni kielelezo kuwa nchi ipo katika njia sahihi ya kujikomboa kiuchumi, kuondoka katika utegemezi wa kuagiza bidhaa kutoka nje kama ilivyodhamiria wakati nchi ikipata uhuru miaka 60 iliyopita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye uzinduzi wa Awamu ya Kwanza ya Kiwanda cha Vifaa vya Umeme cha Elsewedy Electric East Africa LTD kilichopo Kisarawe II Kigamboni jijini Dar es Salaam leo Desemba 6, 2021.

Aidha, Mhe. Rais Samia amesema kiwanda hicho ambacho kitakuwa na uwezo kwa kuzalisha tani 15,000 za nyaya za umeme, transfoma 1,500 na mita 100,000 za umeme kwa mwaka zitakazotumika nchini na kuondoa utegemezi wa kununua bidhaa hizo nje ya nchi na nusu ya bidhaa hizo zitauzwa katika masoko ya nje na kuongeza fedha za kigeni.

Mhe. Rais Samia ameziagiza wizara na taasisi zinazohusika na masuala ya uwekezaji kuhakikisha zina wawezesha na kuweka mazingira mazuri katika sekta hiyo badala ya kuwawekea vikwazo na kuwakatisha tamaa.

Pia, Mhe. Rais Samia amewahakikishia wawekezaji zaidi ya 100 kutoka nchini Misri kuwa, Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini pamoja na mitaji na soko kwa bidhaa watakazozalisha ikiwemo uwepo wa rasilimali watu wenye uzoefu kwa ajili ya kutumika kwenye uwekezaji wao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua rasmi Awamu ya Kwanza ya Kiwanda cha Vifaa vya Umeme cha Elsewedy Electric East Africa LTD kilichopo Kisarawe II Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Mhe. Rais Samia ameagiza Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) kujenga ushirikiano na Kituo cha Uwekezaji cha Misri ili kujifunza mazuri kutoka kwao kwa lengo la kuboresha kama alivyojionea utendaji kazi wa Kituo hicho cha nchini Misri wakati alipofanya ziara nchini humo.

Vilevile, Mhe. Rais amewataka watendaji wa Serikali wanaohusika kuhakikisha wanakamilisha taratibu za upatikanaji wa ardhi katika eneo hilo kwa kuzingatia sheria ili wawekezaji hao waendelee na ujenzi wa mji wa viwanda ambao unatarajiwa kutoa ajira na kuchangia uchumi wa nchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Rais wa Kampuni ya Elsewedy, Bw. Ahmed Elsewedy, Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji),Mhe. Geoffrey Mwambe (kulia), wakati wa uzinduzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Kiwanda cha Vifaa vya Umeme cha Elsewedy Electric East Africa LTD kilichopo Kisarawe II Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasalimia wananchi wa Kibada Wilaya ya Kigamboni alipokuwa njiani akielekea Kisarawe II kwa ajili ya kuzindua Awamu ya Kwanza ya Kiwanda cha Vifaa vya Umeme cha Elsewedy Electric East Africa LTD kilichopo Kisarawe II Kigamboni, Jijini Dar es Salaam leo Desemba 6, 2021

Akiwa njiani kuelekea kiwandani hapo, Mhe. Rais Samia alipata fursa ya kuwasalimia wananchi wa Kibada Wilayani Kigamboni na kuwaahidi kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo changamoto ya maji, umeme na barabara.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Samia amemuapisha Profesa Adelardus Lubango Kilangi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazil na kumtaka kutumia fursa za uwekezaji zilizopo nchini humo katika sekta za kilimo, utalii na michezo ili kuinufaisha Tanzania kupiga hatua zaidi katika maendeleo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Prof. Adelardus Lubango Kilangi kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Barazil leo Desemba 6, 2021 Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akiwa katika picha ya pamoja na Prof. Adelardus Lubango Kilangi mara baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Barazil leo  Desemba 6,2021 Ikulu jijini Dar es salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news