Mtanzania Ericson Temu aanza kuchezesha soka nchini Uingereza

NA MWANDISHI MAALUM

MTANZANIA Ericson Temu amekuwa mwamuzi wa kwanza kutoka nchini Tanzania kuchezesha mchezo wa soka nchini Uingereza.
Temu mwenye umri wa miaka 26 amechezesha mchezo wake wa kwanza kama mwamuzi wa kati kwa umaridadi mkubwa mwishoni mwa wiki aliposimamia pambano la vijana chini ya umri wa miaka 23 baina ya Charlton Athletics na QPR.

Temu mkazi wa mkoani Arusha alisoma elimu yake ya msingi na sekondari katika Shule ya St.Jude iliyopo mkoani Arusha kabla ya kuelekea nchini Mauritius kwa masomo ya juu na baadaye nchini Uingereza.

Akiwa St.Jude nchini Tanzania alianza kusomea kozi za awali za urefa zilizokuwa zikitolewa na Chama cha Soka Mkoa wa Arusha kwa nyakati tofauti.

Temu amesema ndoto yake ni kuchezesha ligi kuu ya soka nchini Uingereza na kwa kiwango alichokionyesha katika mchezo wake wa kwanza anaamini hilo litawezekana ndani ya muda mfupi huku chama cha marefarii kikiahidi kumpangia michezo mingine.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news