Shaka ana kwa ana na viongozi wastaafu CCM katika kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Brigedia Jenerali Moses Nnauye

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, wabunge na viongozi kadhaa wa vyama vya siasa Desemba 5, 2021 wakiongozwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wameshiriki kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya Brigedia Jenerali Moses Nnauye.
Viongozi hao ni kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar, waasisi wa TANU na ASP, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wastatafu, Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba, Mawaziri Wastaafu, Makatibu Wakuu Wastaafu wa CCM akiwemo Mzee Kinana, Makamba na Mkama.
Brigedia Jenerali Moses Nnauye aliyezaliwa Machi 7,1937 na kufariki Desemba 6,2001 ni miongoni mwa wapigania Uhuru wa Tangayika wenye historia ndefu.

Mzee Nnauye alikuwa mwanamuziki mzuri na alitumia sanaa ya muziki katika harakati za kupigania uhuru.
Pia alianzisha na kuendeleza vikundi vingi vya kwaya, taarab na bendi na wasanii wengi waligunduliwa nae na kulelewa kama watoto wake kutokana na kutaka waendelee katika muziki.

Leo ni kumbukizi ya miaka 20, tangu atwaliwe hapa Duniani. Hakika wazalendo wa Taifa hili wataendelea kumkumbuka daima.

Post a Comment

0 Comments