Aliyegusa maisha ya Wema Sepetu 'avuliwa nguo'

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MKUU wa Wilaya wa Temeke mkoani Dar es Salaam, Mheshimiwa Jokate Mwegelo ameingilia kati sakata linalomuhusisha mrembo Wema Sepetu na mfanyabiashara Aristotee ambaye huwa anajiita Chawa wa wasanii maarufu nchini.
DC huyo amesema kuwa, kitendo alichokifanya mfanyabiashara huyo si sahihi na kutaka sheria zichukuliwe ili kukomesha tabia za namna hiyo nchini.

Januari 30, 2022 ilisambaa video iliyomuonesha mfanyabiashara huyo ambaye alisikika akimlinganisha Wema na msanii Irene Uwoya huku akisema kuwa kwa sasa Wema Sepetu amefulia na kwamba hali yake kiuchumi si nzuri akidai hana gari na kwamba amekuwa akiita UBA kila anapotaka kutoka nyumbani.
Aidha,baada ya kipande hicho kusambaa mitandaoni Wema alionekana kuchukizwa ambapo aliamua kutoa ya moyoni kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuingia live katika mtandao huo ambao alionekana akiongea kwa uchungu huku akilia machozi na kuwataka watu kuacha kumzungumzia vibaya na kufuatilia maisha yake.

Kutokana na hali hiyo, leo Januari 31,2022 DC Jokate kupitia mtandao wake wa kijamii ya Instagram ameandika kuwa;

“Ifike muda sheria ifuate mkondo wake kukomesha tabia na hulka za aina hii kwenye jamii zetu. Iwe funzo kwa wote na msamaha pekee yake hautoshi. Watu wanajiua kwa kuwa bullied online. This has to stop!!!,"ameeleza.

Pia hali hiyo imeonesha kuwasononesha na kutopendezwa na kitendo hicho watu mbalimbali na kumtaka Aristostee kuacha tabia hiyo ya kuwasema na kulinganisha watu.

Miongoni mwao ni msanii wa filamu, Irene Uwoya ambaye ameonekana kusikitishwa na kauli ya Aristotee.
“Nimeona niongee, na nataka niliweke hili wazi na kila mtu aelewe since najikuta nahusishwa kutokana na ukaribu wangu na Aristote, Binafsi Nimesikitishwa sana na maneno yasiyo ya kibinaadamu yaliyotolewa na Aristote dhidi ya Wema, Watu waelewe kitu kimoja leo, Sijawahi kumtuma Aristote amtukane Wema wala mtu yeyote yule, sina ugomvi na Wema na sina sababu ya kufanya upuuzi wa namna hiyo, Nimempigia pia Aristote kuoneshwa kukasirishwa kwangu, na niseme tu hiyo ni MIHEMKO yake yeye, sihusiki na lolote juu ya hayo aliyoyaropoka ambayo yanaleta hata uchonganishi baina yetu kitu ambacho sikifurahii kwakweli, kingine nichukue nafasi hii kukupa Pole Wema kwa haya yaliyotokea, hata mimi ningekuwa wewe ningejiskia kama unavyojiskia, pole sana sana, na zaidi Aristote nathamini upendo wako kwangu lakini ningeheshimu sana kama itabaki sisi na maisha yetu bila kunilinganisha wala kunishindanisha na yeyote yule sababu mimi naishi maisha yangu siko kwenye mashindano na mtu, asanteni wote, One love!!,” ameandika Irene.



Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news