CCM Pwani yasema hatua ya Spika Ndugai kukiri mapungufu si kujidhalilisha bali kujiimarisha

NA ROTARY HAULE

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani kimepongeza hatua ya Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai kwa kutoka hadharani kwa kumuomba radhi Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kauli yake tata aliyoitoa hivi karibuni juu ya suala la mikopo ya nchi.

Aidha,chama kimesema kitendo kilichofanywa na Spika Ndugai ni cha kijasiri na kiungwana na kwamba chama kinaamini kukiri mapungufu siyo kujidhalilisha bali ni kujiimarisha.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Ramadhani Maneno,ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho zilizopo Mjini Kibaha.

Maneno amesema kuwa, takribani wiki moja sasa jambo hilo limeleta taharuki ndani ya chama na nchi kwa ujumla kuhusu kauli zilizotolewa na Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Nimewaita leo hii,kwa jambo moja ambalo takribani wiki moja sasa imeleta hataruki ndani ya Chama chetu na kwa Nchi kiujumla kuhusu kauli zilizotolewa na Mheshimiwa Job Ndugai Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,"amesema Maneno.

"Nachukua fursa hii kumpongeza Spika kwa kutoka hadharani na kutoa ufafanuzi juu ya kauli yake na kwenda mbele zaidi kwa kumuomba radhi Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na wananchi wa Tanzania kwa usumbufu wowote uliojitokeza kuhusu kauli yake juu ya suala la mikopo ya nchi,''amesema Maneno.

Maneno amewaomba wana CCM na Watanzania kuiamini kauli yake sambamba na kuendelea kumuunga mkono Rais Samia kwakuwa anafanyakazi kubwa ya kuwatumikia wananchi na kuiletea nchi maendeleo.
 
Januari 3, mwaka huu Spika wa Bunge Job Ndugai,alimuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassan baada ya kuzungumza maneno ya kuvunja moyo juu ya mikopo ya Serikali huku akisema hakukuwa na lolote la kurudisha nyuma juhudi za Serikali Wala hakuwa na nia ya kukashifu juhudi za Serikali katika kutimiza azima ya maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news