Chuo Kikuu Huria wafungua milango kwa wahitimu Kidato cha Nne 2021 wenye 'pass' nne,watoa ofa kabambe

NA MWANDISHI MAALUM

CHUO Kikuu Huria cha Tanzania ambacho kimebobea katika kutoa elimu masafa kimewakaribisha wahitimu wa Kidato cha Nne 2021 wenye pass nne kwa ajili ya kujiunga nao muhula wa masomo mwezi Aprili 2022.

Wito huo umetolewa leo Januari 16,2022 jijini Dar es Salaam na Dkt.Mohamed Omary Maguo ambaye ni Mhadhiri na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

"Awali ya yote tunapenda kuwapa kongole na pongezi nyingi sana kwa jitihada zenu katika masomo zilizowawezesha kuhitimu na kufuzu vizuri katika masomo yenu. 
"Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinawakaribisha wahitimu wote waliopata Pass Nne za kuanzia kiwango cha D kujiunga na Certificates za chaguo lao zinazotolewa hapa Chuoni. Certificates hizo ni:

1. Certificate in Business Administration


2. Certificate in Accountancy


3. Certificate in Procurement and Supply


4. Certificate in Hair and Beauty Therapy


5. Certificate in Youth Work


6. Certificate in Information and Communication Technology


7. Certificate in Library and Information Studies


8. Certificate in Poultry Production and Health


9. Certificate in Social Work 


10. Certificate in Entrepreneurship


11. Certificate in Monitoring & Evaluation


CERTIFICATE YENYE SIFA MAALUMU 

1. Certificate in Early Childhood Care and Education (Muombaji awe na _Division_ 3 ya _Form_ _Four_ na kuendelea au mtu ambaye tayari ni Mwalimu. Hii ni Programu pekee ambayo sifa za kujiunga ni tofauti na _Certificates_ nyingine zote.)

Programu hizi za _Certificate_ husomwa kwa mwaka mmoja wa masomo ambao ni sawa na miezi tisa (9) na mara baada ya kuhitimu, mhitimu hujiunga na Diploma katika fani yake.

"Wapendwa wazazi na wahitimu, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kina matawi katika mikoa yote ya Tanzania Bara na katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Hiki ni Chuo Kikuu cha Serikali kilichoanzishwa kwa sheria ya Bunge namba 17 ya mwaka 1992. Tunawaomba mfike kwenye matawi yetu kwa huduma za udahili ambazo hufanywa Bure bila ya malipo yoyote. Pia, maombi yanaweza kutumwa moja kwa moja kupitia www.out.ac.tz

"Ada ya Certificate zetu ni nafuu sana ambapo kwa mwaka mzima ni Laki Nane (800,000/=) tu. Ada hii inalipwa kwa awamu mbili, yaani 400,000/= kwa awamu moja. Pia, inaruhusiwa kusoma kwa Miaka 2 na Ada hiyo hiyo bila nyongeza yoyote.

"Wapendwa wazazi, tunawasihi muwalete watoto wenu Chuo Kikuu Huria cha Tanzania wapate elimu bora na tena kwa gharama nafuu. Mtoto wako atasoma akiwa anatokea nyumbani na hivyo hakuna gharama za hosteli. 

Maombi yanapokelewa sasa hivi kwa ajili ya Muhula wa APRILI 2022. Hakuna haja ya kupoteza muda kwani mwezi Aprili 2022 masomo yanaanza katika vituo vyetu vyote nchi nzima. 

"Kumbuka wahitimu wa Kidato cha Nne wa miaka ya nyuma wenye ufaulu wa Pass Nne nao pia wanapokelewa.Kwa maswali na ushauri usisite kutuandikia ujumbe mfupi kupitia 0719017254,"amefafanua kwa kina Dkt.Mohamed Omary Maguo ambaye ni Mhadhiri na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na.17 ya mwaka 1992. Ni taasisi ya mfumo mmoja inayotoa kozi ya Cheti, Diploma na Digrii kupitia elimu ya masafa. OUT inaendesha shughuli zake kwa kutumia vituo vya mikoa yote na vituo vya mafunzo zaidi ya 60. Kwa maelezo zaidi fungua tovuti ya https://www.out.ac.tz/ 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news