Hifadhi ya Taifa Mkomazi yaongeza huduma za malazi kwa watalii

NA MWANDISHI MAALUM

HIFADHI ya Taifa Mkomazi imefungua kambi mpya ya malazi kwa ajili ya watalii wanaotembelea hifadhi hiyo.
Hayo yamebainishwa leo Januari 16, 2022 na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi -Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Pascal Shelutete. 

Amesema, kambi mpya imefunguliwa katika eneo la Watershed na ni mojawapo ya mkakati wa kukabiliana na huduma za malazi kufuatia kuzindukiwa kwa Utalii wa Faru hivi karibuni.
"Utalii wa Faru umeonekana kupokelewa vizuri na wadau na hivyo kuwepo na dalili njema za ongezeko la watalii,"amefafanua Kamishna Shelutete.
Kuhusu Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi

Kwa mujibu wa Tovuti Kuu ya Serikali, hifadhi hii, ipo chini ya miteremko ya Safu ya Milima ya Tao la Mashariki inayovutia ya Usambara na Upare yenye nyasi za kijani na kuonekana kwa mbali kutoka kilele cha milima Kilimanjaro chenye theluji.

Mkomazi ni hifadhi isiyoharibiwa inayoonyesha mvuto wa pekee na hazina za kimaumbile na eneo kubwa la wazi-huongeza kutimiza matarajio makubwa ya raha ya mgeni- ni kiungo kinachohitajika sana kati ya vivutio vya ukanda wa Kaskazini na mwambao. 

Ipo Kaskazini mwa Tanzania katikati kwa kugawa mkoa wa Kilimanjaro na Tanga yenye ukubwa wa kilomita za mraba 3,245 (maili za mraba 1,240). 

Hifadhi hii inapakana pia na Hifadhi ya Taifa ya Tsavo magharibi nchini Kenya. Mlango wa kuingilia wa Zange upo kilomita 112 (maili 69) kutoka Moshi, kilomita 550 (maili 341) kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere- Dar es Salaam; Kilomita 142 (maili 88.7) kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa, kilomita 120 (maili 75) kutoka Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro- paa la Afrika na Kilomita 6 (maili 3.7) kutoka mji wa Same. 

Kila siku, maelfu ya watu hupita ndani ya kilomita chache za Mkomazi katika mojawapo ya barabara kuu zenye pilikapilika nyingi nchini Tanzania. Watu hawa na watalii wa ukanda wa kaskazini- hivi sasa wanakaribishwa kwa mikono miwili kuvumbua hazina za habari hii ya milima ya nusu savana yenye ukame- maskani ya makundi makubwa ya twiga, pofu, kongoni, pundamilia, nyati na tembo. 

Mkomazi ni maskani muhimu kwa aina mbili za spishi zilizohatarini kutoweka, vifaru weusi wanaotembea kwa madaha, na mbwa mwitu wapole wa Kiafrika, ambao walirudishwa kwenye hifadhi kwa mafanikio miaka ya 1990. Wakiwa na tabia ya kuhamahama, mbwa mwitu hawa wanaonekana kila mahali, katika hifadhi, lakini vifaru weusi wako katika eneo maalumu lenye uzio, kuwahakikishia kutunzwa kwa usalama kwa burudani ya vizazi vijavyo na ustawi. 

Mkomazi ina spishi nyingi za nchi kavu ambazo ni nadra sana kupatikana mahali pengine popote nchini Tanzania; spishi hizi ni pamoja na choroa wa pembezoni wenye masikio, mgongo mrefu- na pembe zilizotanda na tandala wadogo wa kupendeza wenye pembe za mzunguko. 

Mnyama wa pekee ni swala wenye shingo nyembamba, kichwa kilichojipanga kiajabu na mwenye tabia ya kusimama wima kwa miguu ya nyuma wakati wa kuchuchuma majani ya mijohoro ambayo wanyama wengine hawawezi kuyafikia. 

Ilikuwa hifadhi ya wanyama tangu 1951, Hifadhi ya Taifa hii mpya imepata jina kutokana na kabila la wapare “Kata ya kutekea maji”, ikimaanisha maji kidogo. 

Ni kituo kizuri kwa wanaotazama ndege wenye spishi zaidi ya 450, miongoni mwao ndege wa maeneo ya ukame kama vile kanga aliyefanana na tai, ndege wengine wakubwa wa nchi kavu kama vile mbuni, hondo hondo, kori bustard, secretary bird na spishi za ndege wanaohamahama kama vile Eurasian roller. 

Jinsi ya Kufika Mkomazi 

Kwa barabara, Mkomazi inafikika kwa urahisi kupitia Same, ipo kwenye barabara kuu ya lami inayounganisha Arusha hadi Dar es Salaam. 

Hifadhi inafikika kwa urahisi pia kwa mpango maalumu kupitia mlango wa Njiro, Kivingo na Umba. 

Pia hifadhi inaweza kufikiwa kwa urahisi kutoka vivutio vya karibu au jirani vya kitalii ya Milima ya Tao la Mashariki, Pwani na Mlima Kilimanjaro. Ndege za kukodi zinapatikana hadi kiwanja kidogo cha ndege cha Kisima.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news