DIRAMAKINI BLOG: HERI YA KUZALIWA MHESHIMIWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

UONGOZI wa DIRAMAKINI BLOG unamtakia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan heri ya kuzaliwa leo Januari 27, 2022. Mungu/Mwenyenzi Mungu amjalie afya njema.
DIRAMAKINI BLOG inaamini kuwa, ni wajibu wetu watanzania kuhakikisha tunazingatia hekima, umoja na amani ambazo ni ngao muhimu kwetu popote pale ili kuweza kudumisha uhuru na umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa.

Hiyo ikiwa ndiyo siri kuu ya kuiwezesha Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na wasaidizi wake kutekeleza mipango yake kwa ufanisi ili kutuletea maendeleo katika jamii na Taifa kwa ujumla.

Sambamba na kufanya kazi kwa bidii na kumtegemea Mungu kwa kila jambo ili aweze kutuongoza katika mipango na malengo yetu iweze kutimia kwa haraka. KWA MARA NYINGINE, HERI YA KUZALIWA MHESHIMIWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN. 

Zawadi ya kipekee leo kwa Mheshimiwa Rais kwa maana ya keki, tumpatie ushirikiano, tumuombee, tufanye kazi kwa bidii, tudumishe umoja na upendo. Hiyo ndiyo keki na zawadi zenye thamani kuliko vitu vyote Tanzania na duniani kwa sasa.

Imetolewa;

Januari 27, 2022 na

Mhariri/ Mkurugenzi

Godfrey Nnko

DIRAMAKINI BLOG

Diramakini Business Limited

Post a Comment

0 Comments