Hatuhitaji ngoma za usiku-DC Kyobya

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MKUU wa Wilaya ya Mtwara, Mheshimiwa Dunstan Kyobya katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) amepiga marufuku uwepo wa ngoma za usiku katika wilaya yake ili kuimarisha ulinzi na usalama.
"Hatuhitaji ngoma za usiku, vibali vyote vya ngoma za usiku havipo, kama mtu ana ngoma zake afanye mchana," amesema DC Kyobya.

Amesema kuwa, kama kuna mtu ana ulazima wa kufanya shughuli yake usiku anatakiwa aombe kibali maalumu kitakachopitia kwa Mkurugenzi wa halmashauri, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Mtwara (OCD) pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

Post a Comment

0 Comments