Katibu Mkuu CCM Taifa akiri kupokea barua ya kujiuzulu Spika Ndugai

NA GODFREY NNKO

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Daniel Chongolo amethibitisha kupokea barua ya kujiuzulu kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Ndugai.

Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa leo Januari 6,2022 na Afisa Habari kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu CCM,Said Said Nguya.

"Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ndugu Daniel G. Chongolo leo tarehe 6 Januari, 2022 amethibitisha kupokea barua ya Mheshimiwa Job Yustino Ndugai (Mb) ya kujiuzulu nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Katibu Mkuu ameeleza kuwa, mchakato wa kumpata Spika mwingine baada ya nafasi hiyo kubaki wazi unaendelea,"imeelezea taarifa hiyo.
Katibu Mkuu CCM Taifa, Daniel Chongolo.

Post a Comment

0 Comments