Madiwani wilayani Nkasi wapitisha Bilioni 34/- makadirio ya bajeti

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa kwa kauli moja limepitisha sh. bilioni 34 ikiwa ni makadirio ya bajeti ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Akiwasilisha makadirio ya bajeti hiyo ofisa mipango wa halmsahauri hiyo, Alfred Lazaro amesema kuwa, halmashauri hiyo imepanga kutumia jumla ya sh. bilioni 34,347,993,091.68 ikiwa ni kutoka vyanzo vya ndani ya halmashauri pamoja na ruzuku kutoka serikali kuu.

Amesema kuwa, sh. bilioni 2,780,391,708.68 zitakusanywa kutoka vyanzo mbalimbali vipya na vya zamani vya ndani ya halmashauri sawa na ongezeko la aslimia 1.35 ukilinganisha na mwaka wa fedha uliopita.

Ofisa mipango huyo amesema kuwa, ruzuku kutoka serikali kuu, halmashauri inatarajia kupokea sh. bilioni 31,567,601,385.00 fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya matumizi ya kawaida kama utawala, shughuli za maendeleo pamoja na mishahara ya watumishi.

Pia amesema kuwa, kwa upande wa wananchi wanatarajiwa kuchangia sh. milioni 712,630,000 ambazo ni michango ya nguvu kazi pia aliongeza kuwa katika halmashauri hiyo kuna kaya 71,263 ambapo kila kaya itachangia fedha kiasi cha sh. 10,000.

Naye mwenyekiti wa halamshauri hiyo,Pankras Maliyatabu amewaomba madiwani kushirikiana na watendaji wa halmashauri kutoa elimu kwa wananchi na kushirikiana katika kukusanya mapato ya halmashauri.

Amesema kuwa, ukusanyaji mzuri na usimamizi wa mapato ndiko kutakako iwezesha halmashauri hiyo kutekeleza miradi ya maendeleo na wananchi wanaona thamani ya kodi wanazolipa tofauti na hivyo watakuwa wakilalamikia tozo mbalimbali kwakua hawaoni faida wanayopata kutokana na kulipa tozo hizo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news