Mifumo ya kielektroniki yachochea makusanyo ya mapato, kuimarisha uchumi Zanzibar

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwepo kwa matumizi ya mifumo ya kielektroniki kumechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la makusanyo ya mapato na kuimarisha Uchumi wa Zanzibar.
Kikosi cha Jeshi la Polisi Wanawake wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) kwa Gwaride la mwendo wa haraka katika Kilele cha maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ,hafla iliyofanyika leo Uwanja wa Amaan jijini Zanzibar. 

Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo katika hotuba aliyotoa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari, ikiwa ni maadhimisho ya kilele cha sherehe za miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, zilizofanyika rasmi katika Uwanja wa Amani jijini Zanzibar leo Januari 12, 2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwapungia mkono wananchi wakati alipoingia katika Uwanja wa Amaan jijini Zanzibar leo katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwapungia mkono wananchi wakati alipoingia katika Uwanja wa Amaan Studium leo katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 58 ya mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipokea salamu ya Heshma ya Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar hafla iliyofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium jijini Zanzibar 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (katikati) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman (kulia) Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Tulia Ackson wakisimama wakati wa kupokea Salamu ya Heshima ya Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar hafla iliyofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium jijini Zanzibar . 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama mara baada ya kupokea salamu ya Heshma ya Vikosi hivyo katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar hafla iliyofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium jijini Zanzibar . 
Vikundi mbalimbali vya maandamano vikipita mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar hafla iliyofanyika leo katika Uwanja wa Amaan jijini Zanzibar.
Kikosi cha Jeshi la Polisi FFU wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) kwa Gwaride la mwendo wa pole pole katika Kilele cha maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,hafla iliyofanyika leo Uwanja wa Amaan jijini Zanzibar.
Kikosi cha Jeshi la Polisi Wanawake wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) kwa Gwaride la mwendo wa pole pole katika Kilele cha maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar hafla iliyofanyika leo Uwanja wa Amaan jijini Zanzibar.
Kikosi cha Jeshi la Mafunzo wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) kwa Gwaride la mwendo wa pole pole katika Kilele cha maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,hafla iliyofanyika leo Uwanja wa Amaan jijini Zanzibar.

Kikosi cha Bendera cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) kwa Gwaride la mwendo wa haraka katika Kilele cha maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ,hafla iliyofanyika leo Uwanja wa Amaan Studium Jijini Zanzibar. 

Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) kwa Gwaride la mwendo wa haraka katika Kilele cha maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ,hafla iliyofanyika leo Uwanja wa Amaan jijini Zanzibar. 
Kikosi cha Jeshi la Kikosi cha Kuzuia Magendo (KMKM) wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) kwa Gwaride la mwendo wa haraka katika Kilele cha maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ,hafla iliyofanyika leo Uwanja wa Amaan jijini Zanzibar.
Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi JKU wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) kwa Gwaride la mwendo wa haraka katika Kilele cha maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ,hafla iliyofanyika leo Uwanja wa Amaan jijini Zanzibar.
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wakiwa katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyikia leo katika Uwanja wa Amaan Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi.
Baadhi ya Maofisa wa Vikosi vya Ulinzi na Wananchi wakifuatilia kwa karibu harakati za kusheherekea Maadhimisho ya Kilele cha miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar sherehe zilizofanyika leo uwanja wa Amaan jijini Zanzibar.
Baadhi ya Maofisa wa Vikosi vya Ulinzi na Wananchi wakifuatilia kwa karibu harakati za kusheherekea Maadhimisho ya Kilele cha miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar sherehe zilizofanyika leo uwanja wa Amaan jijini Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mstaafu, Mhe.Dkt.Mohamed Gharib Bilali na Mkewe wakati walipowasili katika Uwanja wa Amaan jijini Zanzibar leo kuhudhuria katika Kilele cha maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais mstaafu wa Zanzibar, Mhe.Dkt.Amani Abeid Karume na Mkewe Mama Shadya karume wakati walipowasili katika Uwanja wa Amaan jijini Zanzibar leo kuhudhuria katika Kilele cha maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemedi Suleiman Abdulla na Mkewe (katikati) wakisindikizwa na wasaidi wao wakati walipowasili katika Uwanja wa Amaan jijini Zanzibar leo kuhudhuria katika Kilele cha maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan (katikati) akiongozana na Wasaidizi wake wakati alipowasili katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar Sherehe zilizofanyika leo Uwanja wa Amaan Studium Jijini Zanzibar.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Marium Mwinyi akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Idrissa Kitwana Mustafa wakati alipowasili katika Uwanja wa Amaan jijini Zanzibar leo katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar .
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali mya jamhuri ya Muungano wa Tanzania walipowasili katika Uwanja wa Amaan Studium jijini Zanzibar leo katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar .

Katika hotuba hiyo, katika kipindi cha Januari – Novemba 2021, Serikali ilifanikiwa kukusanya jumla ya shilingi Bilioni 745.1, ikiwa sawa na ongezeko la asilimia 22, ikilinganishwa na makusanyo ya shilingi Bilioni 610.5 zilizokusanywa katika kipindi kama hicho mwaka 2020.

Alisema mafanikio hayo yamekuja kutokana na uamuzi wa Serikali wa kuanza kutumika kwa mifumo ya kielektronik katika ukusanyaji wa mapato kwa kuunganishwa na taasisi mbali mbali za Serikali pamoja na wafanyabiashara.

Dkt. Mwinyi alisema moja ya mafanikio ya Uongozi wa awamu nane ni kuendelea kuwepo kwa umoja, amani na mshikamano hapa nchini, jambo ambalo limekuwa chachu ya maendeleo katika sekta zote, mbali na kuwepo kwa janga la maradhi ya Uviko -19 ambayo yameathiri uchumi wa mataifa yote Duniani.

Alisema katika kipindi cha Robo ya kwanza ya mwaka 2021 (Januari – Machi) hali ya uchumi wa Zanzibar ulikuwa kwa wastani wa asilimia 2.2, ikilinganishwa na asiliia 1.8 ya kipindi kama hichio mwaka 2020, wakati ambapo katika Robo ya Pili (April – June) uchumi uliimarika kwa wastani wa asilimia 6.5 ikilinganishwa na asilimia 1.4 ya kupindi kama hicho 2020.

Alieleza kuwa katika kipindi cha tatu cha Julai –Septemba 2021, hali ya uchumi iliimarika kwa wastani wa asilimia 8.8 wakati katika mwaka 2020 ulikuwa asilimia 3.3, na kusema ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa miradi ya Uwekezaji pamoja na kuimarika kwa sekta ya Utalii pamoja na shughuli za biashara.
 
Alieleza kuwa Serikali ilifanya juhudi kubwa kudhibti mfumko wa bei,ikiwa pamoja na kuweka bei elekezi kwa bidhaa muhimu, hatua iliyowezesha mfumko wa bei kufikia wastani wa asilimia 1.7 katika kipindi cha Januari – Novemba 2021, ikilinganishwa na wastani wa asilimia 3.4 kwa kipindi kama hicho cha mwaka 2020.

Sambamba na hayo, alisema katika kipindi cha Novemba 2020 hadi Disemba 2021, Serikali kupitia Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) ilisajili miradi 120 yenye thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 787, ambapo unatarajiwa kutoa ajira zipatazo 7,000, huku akibainisha kuwepo Wawekezaji katika Visiwa 10 vilivyotangazwa kuwekezwa, ambapo jumla ya Dola Milioni 261 zinatarajiwa kuwekezwa kwenye visiwa hivyo. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Amani Zanzibar kwa ajili ya kuhudhuria Madhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Viongozi mbalimbali wastaafu alipowasili katika Uwanja wa Amani Zanzibar kwa ajili ya kuhudhuria Madhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Akizungumzia matumizi ya Fedha za Mikopo kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Mkakati maalum wa kuondoa mdororo wa Uchumi, Dk. Mwinyi alisema Serikali imefikia hatua nzuri ya kutekeleza miradi iliopangwa, na kubainisha fedha hizo Shilingi Bilioni 231, zitatumika katika miradi ya Afya, Elimu, Uwezeshaji pamoja na Maji na Nishati.

Rais Dkt. Mwinyi amesema Serikali iko katika mazungumzo ya kupata mkopo wenye thamani ya shilingi Bilioni 230 ili kuziingiza katika uchumi na kuondoa mdororo uliopo.

Amesema, Serikali imeendeleza juhudi za kuimarisha sekta ya Utalii na kuitangaza Zanzibar,ambapo tayari imeandaa na kurahisisha ushiriki wa taasisi za Serikali na Kampuni binafsi katika maonesho, mikutano na makongamano ndani na nje ya nchi, hatua iliyowezesha kuongeza idadi ya watalii kutoka 260,644 (2010) hadi kufikia 393,512,ikiwa sawa na ongezeko la asilimia 50.97.

Ameongeza kuwa, hatua hiyo imewezesha kuongezeka kwa idadi ya Kampuni za Ndege zinazofanya safari za kuja Zanzibar kutoka 27 hadi kufikia 34, huku ikikadiriwa ndege hizo kuleta zaidi ya watalii 50,000 kwa mwaka.

Aidha, amesema serikali imeendelea kufanya juhudi ili kuhakikisha sekta ya Viwanda inaimarika, hatua iliyowezesha mchango wa sekta hiyo katika Pato la Taifa kuongezeka kutoka asilimia 18.1 mwaka 2020 hadi kufikia asilimia 19.6 mwaka 2021.

Amesema katika mwaka 2021 jumla ya Viwanda sita vimezinduliwa na vitatu kuwekewa mawe ya msingi, ambapo kwa ujumla viwanda hivyo vinatarajiwa kutoa wastani wa ajira zipatazo 400.

Kuhusiana na Uchumi wa Buluu (Uvuvi, Mafuta na Gesi), Dk. Mwinyi alisema katika kutekeleza mpango mkakati, Serikali imekamilisha na kutunga sheria ya sera muhimu kwa maendeleo ya uchumi huo,sambamba na kuandaa mpango endelevu wenye thamani ya Shilingi Bilioni 149 kwa ajili ya kuwawezesha wadau, wakiwemo Wavuvi na wafugaji wa mazao ya baharini.

Aidha, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) inakamilisha ujenzi wa Diko na Soko jipya la samaki katika eneo la Malindi kwa thamani ya Shilingi Bilioni 24.

Rais Dkt. Mwinyi amesema kuwa, fedha hizo zimechangwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyotowa shilingi Bilioni 3.6 na Serikali ya Japani iliyochangaia shilingi Bilioni 21.4, ambapo soko la kisasa litawekewa miundombinu ya mitambo ya barafu na kuweza kuwahudumia wafanyabiashara na wananchi wasiopungua 6,500 kwa wakati mmoja.

Aidha, amesema serikali imefanikiwa kupata jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 8.8 kutoka Dola Milioni 58.8 zilizotolewa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo (IFAD) kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zitakazotumika katika utekelezaji wa mradi wa kuweka miundombinu ya Usarifu wa samaki, kuendeleza soko la Mwani pamoja na kujenga Vituo viwili vya kutolea taaluma ya Uvuvi Unguja na Pemba, sambamba na ununuzi wa Meli nne,ili kuongeza uzalishaji wa samaki.

Kwa upande wa sekta ya mafuta na gesi, Dkt. Mwinyi amesema Mwekezaji amekamilisha awamu ya kwanza ya utafutaji wa mafuta na gesi asilia kwa njia ya 2D, ambapo hivi sasa anaendeleza mchakato wa utafutaji mafuta na gesi asili kwa njia ya 3D katika maeneo ya bahari na nchi kavu katika visiwa vya Unguja na Pemba. 

Sambamba na hatua hiyo, ameeleza kuwa Mamlaka ya Usimamzi ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa mafuta na gesi asilia (ZPRA) inaendelea na matayarisho ya ugawaji wa vitalu vipya kwa ajili ya kufungua maeneo mapya ya uwekezaji.

Katika hatua nyingine, amesema katika kipindi cha mwaka 2021, Serikali imefanya juhudi kubwa ya kuendeleza miundombinu ya barabara kwa kufanikisha ujenzi wa barabara za Kinduni – Kichungwani – Kitope (km 4) na barabara ya Sharifumsa- Mwanyanya- Bububu skuli (km 3.8) kwa kiwango cha lami. 

Amesema, barabara za Kwahajitumbo - Mlandege hadi Mbuyu Taifa na barabara ya Hospitali ya Global – Mnazi mmoja zimefanyiwa matengenezo makubwa.

Vile vile amesema, Serikali imeingia mkataba na mkandarasi wa ujenzi wa barabara za ndani zenye urefu wa kilomita 300, ikiwemo ujenzi wa barabara ya Wete – Chake (km 22.1) na kubainisha kukamilika kwa kazi ya upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa barabara mbalimbali zikiwemo za Kitogani – Paje (km. 11), Mahonda – Donge – Mkokotoni (km .13), Dunga – Kipilipini – Pongwe hadi Chwaka Spur (km.30) pamoja na Kinyasini- Kiwengwa (km.13). 

Nyingine, ni pamoja na barabara ya Mshelishelini – Pwani Mchangani (km.7.5), Muyuni- Nungwi (km.12) na Kizimkazi – Makunduchi (km. 13) na kusema hatua ya kutafuta fedha kwa ajili ya barabara hizo kutoka kwa washirika wa maendeleo inaendelea.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud alipowasili katika Uwanja wa Amani Zanzibar kwa ajili ya kuhudhuria Madhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika leo tarehe 12 Januari, 2022. (PICHA NA IKULU).

Katika shamrashamra za Maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi yenye kauli mbiu, “Uchumi wa Buluu kwa Maendeleo Endelevu”, jumla ya miradi 30 imefunguliwa na 13 kuwekewa mawe ya msingi.

Post a Comment

0 Comments