Mwanahabari Fumbuka Ng’wanakilala ateuliwa kuwa Mkurugenzi mpya wa Taasisi ya MISA TANZANIA

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MWANAHABARI mkongwe nchini Fumbuka Ng’wanakilala ameteuliwa kuwa Mkurugenzi mpya wa Taasisi ya MISA TANZANIA.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 31, 2022 na Bodi ya Uongozi MISA TANZANIA. 

MISA Tanzania ni taasisi isiyo ya kiserikali, isiyoegemea upande wowote na isiyo ya faida iliyoanzishwa miaka kadhaa kwa ajili ya kukuza uhuru wa kujieleza nchini.

"Bodi ya Uongozi wa MISA TANZANIA inapenda kuwajulisha wadau wa maendeleo na umma kwa ujumla kuwa imeteua ndugu Fumbuka Ng’wanakilala kuwa Mkurugenzi mpya wa Taasisi ya MISA TANZANIA kuanzia tarehe 1 Februari mwaka 2022. 

"Bwana Fumbuka ni mwandishi mwandamizi, mhariri na kiongozi ndani ya vyombo vya habari ndani na nje ya nchi mwenye uzoefu kwenye tasnia ya habari kwa zaidi ya miaka 20. 

"Tunaomba wadau wetu na wananchi kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake,"imeeleza sehemu ya taarifa hiyo. 

Post a Comment

0 Comments