Rais Dkt.Mwinyi asisitiza umuhimu wa wataalamu wa sheria wenye ujuzi nchini

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwepo kwa wataalamu wa sheria wenye ujuzi ni muhimu katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kijamii nchini.

Dkt. Mwinyi amesema hayo katika hafla ya ufunguzi wa jengo la Mahakama Kuu, lilopo Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) na Marais wastaafu wa Zanzibar na viongozi mbalimbali wakipata maelezo kutoka kwa Mrajis wa Mahakama Kuu ya Zanzibar. (Picha zote na Ikulu).

Amesema, juhudi za Serikali za kuimarisha majengo na upatikanaji wa vifaa, hazina budi kuambatana na utoaji wa mafunzo, ambapo wafanyakazi wa kada ya sheria watapata fursa ya kushiriki ndani na nje ya nchi na hivyo kufanikisha dhamira ya kukuza uchumi.

Amrsema, wataalamu wa sheria wanapaswa kuishauri Serikali katika masuala muhimu mbalimbali muhimu ya maendeleo, ikiwemo uandaaji wa mikataba mbalimbali na taasisi za Kimataifa. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi (kushoto) wakisalimiana na viongozi wakuu walipofika katika sherehe ya Ufunguzi wa jengo la Mahakama Kuu ya Zanzibar,Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja leo ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Ameeleza kuwa, kukamilika kwa ujenzi wa jengo hilo ni hatua muhimu katika kutekeleza azma ya Serikali ya kuweka mazingira bora ya kufanyia kazi katika Utumishi wa Umma, kama ilivyobainisha katika mkakati wa mabadiliko katika Utumishi wa Umma wa 2010.

Dkt. Mwinyi amesema, kwa miaka mingi Mhimili wa Mahakama ulikuwa ukikabiliwa na changamoto ya ufinyu wa nafasi na uchakavu wa majengo, mengi yakiwa yamerithiwa kutoka kwa Wakoloni, ikiwemo Jengo la Mahakama Kuu lililopo Vuga jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhet.Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa tatu kushoto) akiondoa kitambaa kama ishara ya ufunguzi wa jengo la Mahakama Kuu ya Zanzibar,Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja leo ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,wengine ni viongozi mbalimbali wakishuhudia tukio hilo.

Amesema, Serikali itaendelea na dhamira yake ya kujenga majengo ya kisasa na kuweka vifaa vya kufanyia kazi vinavyoendana na mabadiliko na mahitaji ya wakati uliopo.

Ametoa wito kwa watumishi wa Umma kutunza vifaa na mejengo yaliiopo katika maeneo yote ya kazi kwa kutambua kuwa ni mali ya wananchi.

Rais Dkt. Mwinyi aliuagiza Uongozi wa Mahakama kuendelea kulitunza jengo la Mahakama liliopo Vuga, huku akisisitiza azma ya Serikali ya kulifanya eneo la Mji Mkongwe kutumika kwa shughuli za utalii, sambamba na kubainisha azma ya Serikali ya kuhamisha ofisi zote za serikali ziliomo katika eneo hilo ili kulifanya eneo hilo kuwa maalum kwa shughuli za Utalii.

Alimshukuru Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Saba Dkt. Ali Mohamed Shein kwa maono na kuja na wazo la ujenzi wa jengo jipya la Mahakama, na kusema uamuzi wake ulikuwa ni wa kimaendeleo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akikata utepe kama ishara ya Ufunguzi wa jengo la Mahakama Kuu ya Zanzibar ya Zanzibar,Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja leo ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,wengine ni viongozi mbalimbali wakishuhudia tukio hilo.

Akigusia changamoto zinazoihusu Mahakama, aliagiza Uongozi wa Mahakama kuendelea kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazoikabili mhimili huo.

Amesema, ujenzi wa jengo hilo ni mikakati ya serikali katika kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi, na kubainisha uwezo wa serikali wa kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kutumia rasilimali zake wenyewe.

“Ujenzi wake umezingatia mahitaji ya wananchi kwa namna tofauti, ikiwemo upatikanaji wa huduma za benki na watu wenye mahitaji maalum,ni imani yangu kuwa watendaji watakaofanyakazi katika jengo hili watafanya kazi kwa kuzingatia uwabikaji na uadilifu,”amesema.
Mrajis wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Mhe.Mohamed Ali Mohamed Shein (kushoto) akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi (katikati) wakati akitembelea sehemu mbalimbali za jengo la Mahkama Kuu ya Zanzibar alilolifungua leo huko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Alisema vifaa na mifumo iliomo katika jengo hilo itawawezesha watendaji kufanyakazi kwa weledi na umakini mkubwa.

Nae, Kaimu Jaji Jaji Mkuu Zanzibar Khamis Ramadhan Abdalla alisema ujenzi wa jengo hilo umekuja kunatokana na jengo la Mahakama Kuu lililopo Vuga kuwa na changamoto nyingi, ikiwemo ya ufinyu wa Ofisi, kutokuwa rafiki kwa jamii ya watu wenye ulemavu pamoja na kutokuwa na mfumo wa Tehama.

Amesema, wakati wa kipindi cha vikao vya Mahakama ya Rufaa, baadhi ya Majaji hulazimika kuchukua likizo ili kupisha Majaji wa Mahakama ya Rufaa kuendelea na majukumu yao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) na Marais wastaafu wa Zanzibar na viongozi mbalimbali wakisimama wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa mara baada ya sherehe ya Ufunguzi wa jengo la Mahakama Kuu ya Zanzibar alilolifungua leo huko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni katika shamrashamra za maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Amesema, changamoto kubwa inayokabili Mahakama katika usikilizaji wa kesi za udhalilishaji ni kwa mashahidi kushindwa kufika Mahakama kutoa ushahidi, huku baadhi ya nyakati wahusika wa kesi hizo wakibainika kufunga ndoa.

Kaimu Jaji Ramadhan, alitumia fursa hiyo kuiomba Serikali kufikiria uwezekano wa kujenga jengo jipya la Mahakama Kisiwani Pemba, kufuatilia lile lilopo hivi sasa katika eneo la Kichungwani Chakechake kuwa katika mazingira yasiofikika kirahisi kutokana na changamoto ya ukuaji wa Mji.

Aidha, Waziri wa Nchi (OR) Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman alisisitiza haja ya watendaji wa Mahakama kuwajibika ipasavyo kiutendaji ili kwenda sambamba na mazingira halisi ya jengo hilo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akitoa hutuba yake katika sherehe ya Ufunguzi wa jengo la Mahakama Kuu ya Zanzibar alilolifungua leo huko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni katika shamrashamra za maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,ambapo viongozi mbalimbali na Marais wastaafu wa Zanzibar walihudhuria hafla hiyo .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akitoa hutuba yake katika sherehe ya Ufunguzi wa jengo la Mahakama Kuu ya Zanzibar alilolifungua leo huko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,ambapo viongozi mbalimbali na Marais wastaafu wa Zanzibar walihudhuria hafla hiyo.
Mtendaji wa Mahakama Kuu Zanzibar Ndg.Kai Mashiri Mbarouk akitoa maelezo ya kitaalamu wakati wa hafla ya ufunguzi wa Jengo Jipya la Mahakama Kuu Zanzibar Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja, ikiwa ni shamrashamra za lusherehekea Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Katika hatua nyingine, akitoa ‘Salamu za mahakama ya Tanzania’, Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Khamis Juma alisema ujenzi wa jengo hilo ni kielelezo cha dhamira ya Serikali katika kuhakikisha mhimili wa Mahakama unawezeshwa, hivyo akaiomba Serikali kuendelea na uwezeshaji huo hadi ngazi za chini.

Alisema jengo hilo ni zuri na linalotoa matumaini katika utoaji wa haki, hivyo akabainisha mtihani unaowakabili watendaji wa Mhimili huo katika kuhakikisha matumaini ya wananchi yanafikiwa, kuendana na mahitaji ya ujenzi wa Uchumi wa Buluu.

Aliwataka Majaji na Mahakimu kujiwekea taratibu za kuwajibika na kuhakikisha jengo hilo linaendana na kasi ya maendeleo ya Zanzibar, huku kuahidi Mahakama Kuu ya Tanzania kuendelea kushirikiana kikamilifu na Mahakama Kuu ya Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe.Haroun Ali Suleiman akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Jengo Jipya la Mahakama Kuu Zanzibar Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Jaji Mkuu wa Mahkama Kuu Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa jengo jipya la Mahakama Kuu ya Zanzibar Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe.Khamis Ramadhan Andalla akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa jengo jipya la Mahakama Kuu ya Zanzibar Tunguu Wilaya ya Kati Unguja, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya jengo hilo Tunguu.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kulia kwake) Rais Mstaafu wa Zanzibar Awamu ya Saba, Mhe.Dkt.Ali Mohamed Shein, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman na (kushoto kwake) Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu Balozi Seif Ali Iddi, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akihutubia katika hafla ya ufunguzi wa jengo jipya la Mahakama Kuu Zanzibar Tunguu, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Majaji wa Mahakama Kuu Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika hafla ya ufunguzi wa jengo jipya la Mahakama Kuu Zanzibar Tunguu Wilaya ya Kati Unguja, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Mapema, Mtendaji Mkuu wa Mahakama Kai Bashiru Mbarouk alisema Jengo hilo la Mahakama Kuu liliopo Tunguu limegharimu shilingi Bilioni 16.8, ambapo fedha zote hizo kwa asilimia mia moja zinatoka katika mfuko wa Serikali. 

Alisema jengo hilo lililojengwa na Kampuni ya Advent Construction Limited limejengwa katika eneo la Ekari 4.3 likiwa ni la Ghorofa nne ambapo msingi wake ni wa Ghorofa saba, ambapo ujenzi wake umezingatia mambo mbalimbali muhimu ikiwemo usalama.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Rais Mstaaf wa Zanzibar Awamu ya Sita, Mhe.Dkt.Amani Karume, baada ya kumalizika kwa hafla ya ufunguzi wa jengo jipya la Mahakama Kuu Zanzibar Tunguu,ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Rais Mstaaf wa Zanzibar Awamu ya Saba Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar.Mhe.Haroub Ali Suleiman, baada ya kumalizika kwa hafla ya ufunguzi wa jengo jipya la Mahakama Kuu Zanzibar Tunguu, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Muonekano wa jengo jipya la Mahakama Kuu Zanzibar Tunguu,lililozinduliwa na Rais Dkt.Mwinyi ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. 

Aidha, ilielezwa ujenzi wa jengo hilo wakati mwingine ulilazimika kusimama kutokana kujitokeza kwa changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa mchanga wenye sifa unaohitajika, pamoja na kuibuka kwa janga la Ugonjwa wa UVIKO-19, hali iliyochelewesha uletaji wa vifaa.

Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja, Hadidi Rashid Hadidi, alisema pamoja na vyombo vya Sheria kufanikiwa katika ushughulikia wa makosa ya udhalilishaji bado uendeshaji wa kesi hizo unakabaliwa na tatizo kubwa kwa baadhi ya wazazi kushindwa kushirikiana na vyombo hivyo vya sheria.

Post a Comment

0 Comments