Rais Samia ateua viongozi mbalimbali leo

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo Januari 4,2022 ameteua viongozi mbalimbali. Mheshimiwa Rais amemteua Dkt.Baghayo Abdhalah Saqware kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA).
Dkt.Saqware ni Mhadhiri Mwanzamizi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA). Pia Mheshimiwa Rais Samia amemteua, Bw.Charles Jackson Itembe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Eneo Maalumu la Mauzo ya Nje (EPZA).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Bw.Itembe ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania (Azania Bank Limited).

Uteuzi mwingine ni wa Bw.Ernest Maduhu Mchanga ambaye Mheshimiwa Rais Samia amemteua kuwa Katibu wa Tume ya Pamoja ya Fedha (JFC).

Bw.Mchanga ni Katibu Msaidizi,Fedha na Utawala, Tume ya Pamoja ya Fedha (JFC) kutoka Wizara ya Fedha na Mipango.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu kupitia taarifa aliyoitoa leo Januari 4,2022 ameeleza kuwa, uteuzi huo umeanza Januari Mosi,2022.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news