Richard Cheyo awalilia waandishi waliofariki katika ajali mjini Busega

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MKUU wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Tume ya Utumishi wa Umma, Richard Cheyo ameeleza kusikitishwa na ajali ya gari iliyoaua waandishi wa habari leo.
"Nimesikitishwa sana na vifo vya Waandishi wa Habari waliofariki leo 11/01/2022 kwa ajali ya gari Kalemela- Busega, wakienda kutekeleza majukumu yao. Natoa Pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na waandishi wa habari. Tunawaombea Mungu Awaweke Mahali Pema,"ameeleza Cheyo.

Ajali hiyo imehusisha magari mawili likiwemo la abiria aina ya Toyota Hiace na jingine lenye namba za usajili STK 8140 mali ya Serikali lililokuwa limebeba waandishi wa habari mkoa wa Mwanza wakitokea Mwanza kuelekea Ukerewe kupitia Bunda, Mara baada ya kugongana uso kwa uso.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, Bw. Emmanuel Luponya Sherembi, alilazimika kuahirisha ratiba ya ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mhandisi Robert Gabriel kwa ajili ya kukabidhi miradi baada ya ajali hiyo.

Post a Comment

0 Comments