TANESCO YATOA TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA UMEME KATIKA BAADHI YA MAENEO NCHINI

NA MWANDISHI MAALUM

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) linawafahamisha wateja wake wa mikoa ya Dodoma, Singida, Shinyanga, Mwanza, Mara, Tabora, Simiyu na Geita, kuwa leo Jumatano Januari 12, 2022, saa 3:00 asubuhi kumetokea kukosekana kwa huduma ya umeme.
SABABU: Hitilafu kwenye kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Zuzu Dodoma.

JITIHADA: Wataalam wetu wanaendelea na jitihada za kurejesha umeme na tutaendelea kutoa taarifa zaidi. 

Tunawaomba radhi wateja wetu kwa usumbufu utakaojitokeza. 

Mitandao ya kijamii:

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetutz, 

Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetutz 

IMETOLEWA NA;

Ofisi ya Uhusiano,

TANESCO MAKAO MAKUU.

Post a Comment

0 Comments