Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Januari 18, 2022

NA GODFREY NNKO

PAUNDI ya Uingereza inabadilishwa kwa Shilingi 3120.635 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3152.766.
Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 360.172 huku ikiuzwa kwa shilingi 363.69 na Yen ya Japan inanunuliwa kwa shilingi 19.96 na kuuzwa kwa shilingi 20.16.

Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.18 na kuuzwa kwa shilingi 2.25 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.65.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Januari 18, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kwa upande wa Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 148.455 na kuuzwa kwa shilingi 149.896 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.17 na kuuzwa kwa shilingi 20.34.
Pia kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania, Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.206.

Dola ya Marekani nchini inabadilishwa kwa Shilingi 2286.515 huku ikiuzwa kwa Shilingi 2309.38.

Kwa mujibu wa BoT, Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2607.99 na kuuzwa kwa shilingi 2635.003.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news