Waziri Dkt.Jafo apiga marufuku shughuli za ufyekaji msitu Kijiji cha Kalangasi

NA MWANDISHI MAALUM, OMR

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo Waziri Jafo amepiga marufuku shughuli za ufyekaji wa msitu katika Kijiji cha Kalangasi wilayani Uyui mkoani Tabora.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya uyui, Kisare Makori alipowasili kikazi katika Kijiji cha Kalangasi wilayani Uyui mkoani Tabora leo Januari 21, 2022 kwa ziara ya kikazi.

Dkt. Jafo amechukua hatua hiyo leo Januari 21, 2022 wakati wa ziara ya kikazi ambapo amebaini kiasi kikubwa cha miti kimeanza kukatwa kwa ajili ya mradi wa kilimo cha korosho.

Akizungumza akiwa katika eneo hilo alionesha kushangazwa na kitendo hicho cha kufyeka msitu na kuhoji kuwa hakuna eneo lingine la kufanya mradi huo akisema kuwa hiyo ni dhuluma kwasababu umehifadhiwa na mababu zetu ili uwe na faida kwa vizazi.

“Wazo la kuanzisha kilimo cha korosho ni zuri, lakini sidhani kama hili jambo mnalotaka kulifanya ni sahihi hasa ukizingatia mimi nikiwa ni mtu niliyepewa dhamana ya kulinda mazingira na msitu huu kama mlivyoeleza katika taarifa yenu uko Manyoni na hapa, ni bora tuliache libaki kuwa eneo la hifadhi, nasema sitaruhusu msitu huu usafishwe,” amesema.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kijiji cha Kalangasi wilayani Uyui mkoani Tabora leo Januari 21, 2022. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Dkt. Batilda Burian.

“Jana tu nilizindua Kampeni ya upandaji miti kwa wanafunzi kote nchi ili kuwafanya wawe na moyo wa kutunza mazingira sasa leo hii sisi wazazi tunaonekana wa kwanza tunaenda kufyeka miti kwa hali ya juukwa lengo la kukabiliana na changamoto hizo,” ameongeza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo (katikati) akikagua eneo la msitu linalofyekwa katika Kjijiji cha Kalangasi wilayani Uyui mkoani Tabora leo Januari 21, 2022. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi  Dkt.Batilda Burian na Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Kisare Makori.(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS).

Aidha, waziri huyo aliuagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuangalia namna ya kuanzisha mradi mkubwa wa ufugaji wa nyuki wa kisasa ili msitu huo unufaishe wanakijiji hao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news