NAIBU WAZIRI SAGINI AAGIZA JESHI LA POLISI KUWAWAJIBISHA ASKARI WANAOKIUKA MAADILI YA KAZI

NA MWANDISHI MAALUM-WMNN

MWENYEKITI wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini ameliagiza Jeshi la Polisi kuwawajibisha askari watakaokiuka maadili kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za kiutendaji. Aidha amelielekeza jeshi hilo kuwapongeza askari wale watakaofanya kazi zao vizuri.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Jumanne Sagini akizungumza na wajumbe wa Sekretarieti ya Usalama Barabarani leo, katika Ukumbi uliopo Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani, jijini Dar es Salaam.

“Nimefadhaishwa na askari wanaokiuka maadili ya kazi. Wale wanaokiuka maadili wawajibishwe kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu ili Jeshi letu la Polisi liendelee kuaminiwa na kuheshimika,” amesema.

Naibu Waziri Sagini alizungumza hayo Februari 21, 2022, katika ukumbi wa Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani jijini Dar es salaam, wakati alipokutana na Sekretarieti ya Usalama Barabarni kwa lengo la kujitambulisha kwa wajumbe wa Sekretarieti hiyo pamoja na kufahamu utendaji kazi wao.

Aidha, Naibu Waziri Sagini ameipongeza Sekretarieti ya Usalama Barabarani kwa kutoa elimu ya matumizi sahihi ya barabara kwa wananchi na kupunguza ajali zinazopelekea vifo, majeruhi na uharibifu wa miundombinu.
Baadhi ya Wajumbe wa Sekretarieti ya Usalama Barabarani wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambae pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, leo aliyetembelea Sekretarieti hiyo iliyopo Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani, jijini Dar es Salaam.

“Ninawapongeza kwa utekelezaji wa majukumu yenu ya kuhakikisha kuna kuwepo hali ya usalama barabarani hasa kwa kutoa elimu kwa Watanzania nakupelekea kudhibiti ajali nchini,”amesema.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, SACP Wilboroad Mutafungwa akizungumza wakati wa Kikao cha Sekretarieti ya Usalama Barabarani na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini leo, katika Ukumbi uliopo Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wajumbe wa Sekretarieti ya Usalama Barabarani, amewataka kuharakisha utekelezaji wa maelekezo waliyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan ya ununuzi wa vitendea kazi kwa kuyapa kipaumbele katika mpango kazi wao.

“Niwahimize, maagizo mnayopewa na Viongozi wenu na yale ambayo tumeagizwa na Mheshimiwa Rais tuhakikishe tunayafanyia kazi haraka,”amesema.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti ya Usalama Barabarani baada ya kikao na Sekretarieti hiyo leo katika Ukumbi uliopo Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani , jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, Naibu Waziri Sagini ameihakikishia Sekretarieti hiyo kuwa, Wizara itaendelea kutoa ushirikiano na kuendela kuzipatia ufumbuzi changamoto zilizopo na zitakazojitokeza kwa lengo la kuhakikisha kuwa, suala la ajali za barabarani linaendelea kupungua.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news