Ajali iliyosababisha kifo cha Profesa Ngowi, dereva wake ilitokea hapa, tazama pia wasifu wake

*Ajali ilitokea Mlandizi mkoani Pwani

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

PROFESA wa Chuo Kikuu cha Mzumbe nchini Tanzania, Honest Ngowi amefariki dunia leo Machi 28,2022.
Hayo ni Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Leo na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Lughano Kusiluka.

"Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Lughano Kusiluka anasikitika kutangaza kifo cha Prof. Honest Ngowi na dereva wake, waliofariki asubuhi ya leo kwa ajali ya gari wakiwa njiani kuja Kampasi Kuu Morogoro.
"Tunaomba muwe watulivu wakati Menejiementi inaendelea kufuatilia taarifa kamili ya tukio hili, na kuweka taratibu zingine. Taarifa zaidi zitatolewa rasmi na taratibu zingine za kuwahifadhi wenzetu. Bwana alitoa na Bwana Ametwaa jina la Bwana lihimidiwe. Poleni Wote kwa msiba huu mzito,"imeeleza taarifa hiyo iliyotewa na Ofisi ya Mawasiliano.

Wasifu wa Profesa Honest Ngowi
Ajali hiyo imehusisha lori na gari ndogo alilokuwa anasafiria Profesa Ngowi kwenda mkoani Morogoro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza imetoka eneo la Mlandizi mkoani Pwani ikihusisha magari matatu.

"Ni kweli ajali imetokea leo saa 12 alfajiri ikihusisha magari matatu aina ya Noah, Land Cruiser alilokuwa anasafiria yeye na lori ambalo ndio chanzo cha ajali lilihama njia na kuiangukia Noah ubavuni kisha kuilalia gari ya Ngowi," amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news