RS Berkane yatozwa faini Milioni 250/- kwa kufanya fujo dhidi ya Simba SC

NA MWANDISHI WETU

SHIRIKISHO la Soka barani Afrika (CAF) limeitoza faini klabu ya RS ​​Berkane ya Morocco faini ya dola za Kimarekani 108,000 (zaidi ya shilingi milioni 250) kwa kufanya vurugu kwenye mechi zote mbili za nyumbani na ugenini dhidi ya Simba SC.
Katika mechi hizo za Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika nchini Morocco mashabiki wa Berkane waliwatupia vitu wachezaji wa Simba katika dimba la Manispaa ya Berkane, Februari 27, mwaka huu ambapo wenyeji walishinda 2-0 na kwa kosa hilo wametozwa faini ya dola 8,000.

Aidha,kwenye mchezo wa marudiano dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, wenyeji Simba ambao waliibuka na ushindi wa 1-0 Machi 13,2022 Makamu wa Rais wa Berkane, Majjid Madrane alivamia uwanjani na kuwaongoza wachezaji wake kuwafanyia fujo marefa.

Kamati ya Nidhamu ya CAF kutokana na kosa hilo,imemfungia Madrane kujihusisha na shughuli zozote za soka zinazotambuliwa na bodi hiyo ya soka barani kwa mwaka mmoja pamoja na kumpiga faini ya dola za Kimarekani 100,000 hivyo kufanya jumla ya dola 108,000.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news