Sherehe za Alama ya Mwaka Mmoja wa Mama (Rais Samia) kutikisa mjini Shinyanga

NA MWANDISHI MAALUM

TAASISI ya Bega kwa Bega na Mama Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na akina mama Wilaya ya Shinyanga Mjini wameandaa Sherehe Maalumu ya Maadhimisho ya mwaka mmoja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan madarakani. Sherehe hizo zitafanyika Mjini Shinyanga Machi 12  hadi 13, 2022.
Katika Sherehe hizo Taasisi ya Bega kwa Bega na Mama Samia Suluhu Hassan imeandaa Matembezi Maalumu siku ya Jumamosi Machi 12,2022 yatakayoanzia Viwanja vya CCM Mkoa wa Shinyanga mpaka uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga.Vile vile taasisi hiyo imeandaa semina kwa wajasiriamali wadogo wadogo na wamachinga, siku ya Jumapili Machi 13,2022 katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini ambapo watapewa elimu juu ya umuhimu wa kupata bima za moto ili kulinda mitaji yao na majanga ya moto.

Wote mnakaribishwa

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news