Wawekezaji kutoka Qatar watua Tanzania

*Kuangazia fursa sekta za mifugo, vifaa tiba, utalii, madawa, anga na uchumi wa buluu

NA MWANDISHI WETU

KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimepokea wawekezaji 24 kutoka nchini Qatar ambao wamekuja kuangalia fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali.
Akizungumza baada ya kuwasili wawekezaji hao Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Bi. Anna Lyimo amesema ujio wa wawekezaji hao ni kufuatia ziara ya viongozi wa TIC nchini Qatar ambapo walikutana na kufanya mazungumzo na wafanyabiashara kutoka Shirikisho la Wafanyabiashara la Qatar (KERALA BUSINESS FORUM).

"Leo tumepokea wafanyabiashara 24 ambao wamekuja kuangalia fursa za kuwekeza kati sekta mbalimbali ikiwemo mifugo, vifaa tiba, utalii, madawa, sekta ya anga pamoja na masuala ya uchumi wa buluu,"amesema Bi. Lyimo.
Amesema, kufuatia uwepo na mazingira mazuri ya uwekezaji nchini pamoja na kukuwa kwa diplomasia nchini imekuwa chanzo cha wawekezaji wengi, hivyo kuwasihi wawekezaji toka ndani ya nchi wajiunge na TIC ili kuweza kupata taarifa mbalimbali za fursa za uwekezaji nchini.

Amesema kuwa, wawekezaji hao wanatarajiwa Machi 29, mwaka huu kutembelea Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ili kuangalia fursa ya uwekezaji, lakini kwa sasa TIC inawapitisha katika taratibu mbalimbali za uwekezaji pamoja na masuala ya vibali vya kuwekeza nchini.
Mapema Rais wa Shirikisho la Wafanyabiashara nchini Qatar, Bw.Shanavas Bava amesema wamekuja kuangalia fursa za kuwekeza hapa nchini kutokana na Tanzania kuwa na fursa nyingi, ikiwemo
mazingira rafiki ya kufanyia biashara.

"Tumekuja kuangalia fursa zilizopo za uwekezaji kufuatia kuridhishwa na uwepo wa mazingira mazuri ya uwekezaji nchini,"amesema Bw. Bava.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news